Waziri mkuu
wa jamuhuri ya muungano wa
Tanzania Mh.kassim majaliwa amewaagiza wakuu wa wilaya nchini kuhakikisha kuwa wanawafatilia watoto wote
ambao walifaulu kujiunga na masomo ya sekondari kuhakikisha wanakwenda
shule.
Ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akipokea taarifa
ya mkoa wa geita juu ya utekelezaji wake wa maendeleo amesema wakuu wa wilaya
wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanasimamia kila mtoto ambaye amefaulu anakwenda
kuanza masomo ya sekondari na kuachana na swala la utoro na kwamba kwa sasa
wazazi hawana sababu ya kuwazuia watoto kusoma kwani elimu
ni bure.
Aidha waziri
Majaliwa ameongeza kuwa ni vyema kuhakikisha kuwa wale wote ambao
wamewasababishia watoto wa kike kutokuendelea kupata elimu kuwachukulia hatua
za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwasaka na kuwafikisha katika ngazi ya sheria.
Akiwakilisha wakuu wa wilaya ,mkuu wa wilaya ya
Nyang’wale Mh.Ibrahimu Malwa,amesema kuwa agizo la waziri mkuu wamelipokea na
kwamba watahakikisha kuwa wanatekeleza kile ambacho kimeagizwa kwa kuhakikisha wanawafatilia watoto ambao
wanajihusisha na maswala ya uchimbaji ili waweze kwenda shule na kwamba wale
wote ambao wamekuwa wakifanya tabia za kuwaajiri watoto watahakikisha wanachukuliwa
hatua za kisheria.
Waziri mkuu Mh.Kassim Majaliwa yupo mkoani hapa kwa
ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo leo ameweza kupokea taarifa ya mkoa na
kuzindua duka la dawa la (MSD) katika hospitali ya wilaya ya Chato na pia
kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara wilayani hapo.
No comments:
Post a Comment