Wakulima
wa zao la pamba katika kata ya Ikunguigazi wilayani Mbogwe mkoani Geita wameilalamikia
serikali kwa kuwaingiza kwenye kilimo cha mkataba ambacho wamekuwa wakikabiliwa
na hujuma nyingi zikiwepo kuuziwa mbegu feki, bei kuwa chini mizani iliyochakachuliwa
na sasa wamesambaziwa dawa za viuatirifu feki ambazo haziui wadudu.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na storm habari wamesema kuwa dawa walizosambaziwa na umwapa
haziuwi wadudu hali ambayo imeendelea
kupelekea zao la pamba kuendelea kuharibika kutokana na kuliwa na wadudu.
Diwani
kata ya Ikunguigazi Lutandula Kazimoto ameiomba Serikali kuhakikisha inakuja
kuchunguza kila shamba na ikiwezekana iwasaidie wakulima wa zao hilo kuwapatia
fidia ya sehemu ambazo zimeharibika kutokana na dawa hizo.
Kaimu Afisa kilimo wilaya ya Mbogwe Stephen Shilemba
amesema kuwa tatizo kubwa la wakulima wanashindwa kufuata
maelekezo na masharti ya uchanganywaji wa dawa wanataka dawa kidogo ipulizie
heka nyingi ili kubana matumizi hivyo shida iliyopo kwa wakulima ni elimu, bado
hawajaelewa wanatumia mazoea hivyo amewataka
kuacha mazoea na ni vyema wakafuata masharti ya kitaalamu.
No comments:
Post a Comment