Naibu waziri wa Nishati na Madini Dkt.Medard Kalemani akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika eneo la tukio.
Mkuu wa mkoa wa Geita Bi. Fatuma Mwasa akizungumza na wananchi waliohudhuria eneo la tukio.
Mkuu wa mkoa wa Geita Bi.Fatuma Mwasa
Baadhi ya wananchi waliohudhuria eneo la tukio.
Wananchi wa kata ya
mgusu iliyopo mkoani Geita wameiomba Serikali kuwafungulia mgodi uliofungwa baada
ya kutokea vifo vya wachimbaji 5 na wengine kujeruhiwa ili kuendeleza shughuli za uchimbaji ambao unawaendeshea
maisha.
Hayo wameyasema
wakati walipokuwa wakizukungumza na mkuu
wa mkoa wa Geita Fatuma Mwasa kwenye
mkutano uliofanyika katika maeneo ya machimbo hayo na kueleza jisi wanavyoathirika
kwa kufungwa kwa mgodi huo.
Kaimu Afisa madini wa
mkoani hapa Bw.Fabian Lukas Mshai
amewaomba wananchi kuzingatia kanuni za
uchimbaji ili kuepuka kukumbwa na maafa mengine.
Aidha mkuu wa mkoa Geita Bi.Mwasa
amewapa pole wananchi hao na kuwataka kumpa ushirikiano na kumuunga mkono ili
kutokomeza vifo katika mgodi huo.
Marchi 9 majira ya saa
tisa alasiri watu watano walifariki na wengine kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na
kifusi wakati walipokuwa kwenye shughuli
za uchimbaji.
No comments:
Post a Comment