Mkazi mmoja wa Kata ya
Mbugani, Manispaa ya Tabora, Mashaka Maziku (60) amehukumiwa kifungo cha miaka
saba jela kwa kosa la kumkata sehemu za siri mkewe kwa imani za kishirikina ili
apate mali.
Hakimu Joctan Rushwela
alisema jana kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora imeridhishwa na
ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka.
Hakimu Rushwela
alisema anamhukumu mshtakiwa huyo kwenda jela ili iwe fundisho kwa wengine
wanaokuwa na tamaa ya kujipatia mali kwa njia za kishirikina.
Awali wakili wa
Serikali, Idd Mgeni alidai kuwa mshtakiwa huyo na mganga wa jadi, walitenda
kosa hilo kati ya Oktoba 29 na Novemba 2, 2014 katika eneo la Kazaroho Kata ya
Mbugani, Manispaa ya Tabora.
Wakati wa tukio hilo,
ilidaiwa kuwa Maziku aliambiwa na mganga huyo ambaye ni mshtakiwa wa pili
katika kesi hiyo, Kahele Paul kwamba akipeleka sehemu za siri za mkewe atapata
Sh milioni 5.
Alidai baada ya kupewa
ushauri huo, alimchukua mkewe na kwenda kumnywesha pombe ili aweze kutimiza
ukatili huo.
Alidai baada ya kunywa
pombe nyingi, alichukua kisu na kumkata sehemu za siri mkewe na kuzihifadhi
kwenye mfuko wa suruali yake na kutoweka.
Alidai kwa mujibu wa
mashahidi wanne, mwanamke huyo alikuwa akipiga kelele kutokana na maumivu
makali aliyopata huku akivuja damu nyingi.
No comments:
Post a Comment