Zoezi la kuhakiki
watumishi hewa lililoamriwa na Rais John Magufuli limemkumba Askari Polisi
aliyeajiriwa mwaka 2003 baada ya kubainika kuwa ametumia vyeti vya kugushi.
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amemtaja Askari huyo kuwa ni Emanuel Nikolas Nyangoli
mwenye namba F5425 Pc ambaye baada ya kutuhumiwa kuwa na vyeti vya kughushi
aliamua kutoroka na hajulikani aliko.
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amesema Askari Emanuel Nyangol amefanya kazi ndani ya
jeshi la Polisi kwa muda wa miaka 13 bila kujulikana kuwa ana vyeti vya
kugushi,
Vielelezo vya
kuonyesha jeshi la polisi lina taarifa kuwa uajiriwa wa askari huyo ni
wakutatanisha ndio ulio mfanya atoroke baada ya kujua jeshi la polisi
lina taka kumfungulia mashitaka
Jeshi la polisi mkoa
wa Ruvuma linawaomba wanchi ambao watakuwa na tarifa za Emanuel Nyangoli watoe
tarifa kwa kituo chochote cha polisi au apige kwa kamanda wa Polisi Mkoa wa
Ruvuma Nomber 0715 009 956.
No comments:
Post a Comment