Wananchi mkoani Geita wametakiwa kujitokeza kwa wingi
kupima magojwa ya kifua kikuu pamoja na virusi vya ukimwi ili waweze
kutambua afya zao.
Hayo
yamesema na mratibu wa mradi wa Challenge TB
mkoani Geita Bw. Patriki Magassa
kutoka katika shirika la KNCV lenye makao makuu yake jijini Dar es
salaam, kwa kushirikiana na wizara ya afya mandeleo ya jamii jinsia,wazee na
watoto kupitia mpango wa taifa wa
kudhibiti kifua kikuu na ukoma nchini,huku akidai lengo la mradi huo ni kuibua
wagonjwa wengi wasiokuwa na mazoea ya
kupima pindi wanapokuwa na dalili za magonjwa hayo.
Ameongeza
kuwa baadhi ya wagonjwa wanapogundulika kuwa na magonjwa hayo wamekuwa wakigoma
kutumia dawa na wengine kutoroka hali
ambayo imekuwa ni changamoto kwa watoa huduma.
No comments:
Post a Comment