Saturday 29 April 2017

WANAFUNZI 11 WASHINDWA KUENDELEA NA MASOMO KUTOKANA NA KUPATIWA MIMBA WILAYANI BUKOMBE

Baadhi ya wanafunzi shule ya Msingi ya Uyovu wakiwa kwenye sherehe za kutimiza miaka Kumi tangu kuanzishwa kwa shule Hiyo


Mgeni rasimi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bukombe pamoja na msafara wakiingia kwenye viwanja vya maazimisho ya sherehe za jubilee yaliyokuwa yakifanyika kwenye viwanja vya shule Hiyo pembeni yake mkono wa kushoto ni mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Nicas Safari.

Msafara ukiingia kwenye viwanja shughuli inapofanyika.

Kwaya ya wanafunzi shuleni hapo ikiingia kutoa Burudani ya uwimbaji.

Wadau mbali mbali wakiwemo walimu pamoja na wazazi wakifuatilia kwa makini shughuli ya uwimbaji iliyokuwa ikiendelea.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ,Nicas  Safari Mayala akijitambulisha mbele ya wanafunzi na wazazi ambao walikuwa wamefika kwenye sherehe Hizo.

 Wanafunzi wa Skauti wakionesha ukakamavu wao kwa kutengeneza mnara kwenda Juu kwa kubebana wao kwa wao.

Skauti wakivunja Tofari lililokuwa tumboni kwa mwanaskauti.

Mwalimu Mkuu wa Shule y Sekondari Uyovu, Saimon Mashauri akielezea mbele ya mgeni Rasmi Makusudi na Malengo ya kuwepo kwa sherehe ya Jubilee ya Miaka Kumi tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.

Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Sekondari Uyovu  Josephat Waka  akielezea changamoto za watoto kukatishwa masomo kutokana na kupigwa mimba wakiwa katika kipindi cha umri mdogo.

Meza Kuu ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe pamoja na Mbunge na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.

Vijana wa Kudesi na Kubugi wakionesha mautundu yao wakati wa sherehe ya miaka kumi ya shule ya Sekondari ya Uyovu.

Mbunge wa Jimbo Bukombe  Dotto Biteko,Akitoa neno la utangulizi na kumkaribisha Mgenu Rasmi kwaajili ya kuzungumza na wazazi wanafunzi na baadhi ya wananchi waliuzulia Hafra hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga akizungumza na wananchi waliofika kwenye Hafra Hiyo ambapo moja kati ya maagizo ambayo ameyatoa ni watuhumiwa kukamatwa ndani ya wiki inayokuja.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe hakigawa vyeti vya pongezi kwa idara ambazo zimefanya vizuri shuleni hapo.



Wanafunzi 11 wote wakiwa wa Sekondari,sita kutoka Uyovu Wilayani Bukombe Mkoani Geita,wamekatishwa masomo yao baada ya kupata ujauzito huku baadhi ya watendaji wa Serikali Idara ya Elimu Wilayani humo wakidaiwa kugeuza mtaji matukio hayo kwa kushirikiana na wazazi,wanaume waliowapa mimba kisha kuyamaliza kimyakimya.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Sekondari Uyovu  Josephat Waka  ambaye ameibua tuhuma hizo mbele ya viongozi mbalimbali wa chama na Serikali akiwemo mkuu wa Wilaya hiyo  na Mbunge wa jimbo hilo  wakati wa Jubilee ya miaka kumi tangu ilipoanzishwa shule hiyo.

“Hadi kipindi hiki kuna mimba sita kwenye shule ya sekondari ya uyovu sisi kama bodi tumejitaidi kupeleka taarifa sehemu husika lakini taarifa ya kusikitisha kuna baadhi ya wazazi watumishi sio waaminifu wamekuwa wakishirikiana na  watu hawa ambao wamewapa watoto mimba mwisho wa siku wanatoroka mimi kama mwenyekiti wa Bodi nilikuwa nimefikilia Jambo moja endapo kama tutawapata chama cha wanasheria wanawake kuja na kutusaidia swala hili naamini tutamaliza tatizo hili maana linasumbua kwa kiasi kikubwa katika maeneo yetu”Alisema Waka.

Hata Hivyo Mwenyekiti wa Bodi ya shule ameongezea kuwa Jitihada ambazo wamekwisha kuzichukua hadi sasa ni kwamba wanampango wa kukaa na wazazi waweze kuchangia ujenzi wa hostel ambazo zinatasaidia kunusuru Mimba za watoto wa kike katika shule.

“Ndugu mwandishi najua kuwa hapa uyovu ni eneo la biashara na mala nyingi kuna mabinti ambao wanaishi mbali na maeneo haya kwa hiyo unakuta wanapanga kwenye makazi ya watu mwisho wa siku wanapopata shida wanarubunika na kujikuta wakiingia kwenye mchezo wa mapenzi hivyo jitihada kubwa tunaona sisi kama Bodi ya shule ni kukutana na wazazi na kuwaomba kuchangia ili tuweze kujenga hostel kwa kushirikiana na serikali”Alisema Waka

Mbunge wa Jimbo hilo Dotto Biteko ambaye alikuwa ameambatana na Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Hiyo,amesikitishwa na taarifa hizo ambapo amechukua nafasi hiyo kuwahasa wanafunzi kuachana na tabia ya kuharakia mapenzi katika umri mdogo.

“Tumeambiwa hapa kuna mimba sita kwenye shule hii Mh Mkuu wa Wilaya Nitashangaa sana endapo kama kuna mtu amemtia  mimba mwanafunzi yupo mitaani hajachukuliwa hatua zozote za kisheria kama kuna mzazi ambaye mtoto wake amepatwa mimba na anakwenda kuonga ili Yule aliyemtia mimba mtoto wake aachiwe huru mimi inaniuma sana unakuta mtoto mdogo ametiwa mimba anaangaika na mtoto lakini mwanaume yeye anaendelea na maisha yake bila shida yoyote ,Nanyinyi wanafunzi tunawaomba msome sio uko shule na wewe unakuwa na maswala ya Bebi subilia wakati wako utafika”Alisisitiza Dotto.

Kaimu Afisa elimu wa Wilaya hiyo  Mwl Leornad Kingwa mbali na kukiri wanafunzi sita wa Sekondari hiyo kukatishwa masomo kwa ujauzito wamedai wamekwishaanza kuchukua hatua huku mkuu wa Wilaya hiyo Maganga akiagiza kufikia wiki ijayo awe amepewa orodha ya majina ya wanaume waliowapa mimba watoto hao ili achukuwe hatua haraka iwezekanavyo ikiwa ni pamoja na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria.

“Changamoto zipo wajawazito wapo wanapatikana kiwilaya wanafunzi takribani kumi na moja wanaujauzito ingawa shule ya uyovu ndio imeonekana kuwa na wanafunzi wengi zaidi tumeshachukua hatuia taarifa zipo kwenye jeshi la polisi tayario”Alisema Kingwa.

Hata hivyo baadhi ya wazazi Julius John na Lucy Malaki pamoja na kumshukuru Mkuu wa wilaya kwa maamuzi ambayo ameyachukua pia wamewaomba watu wenye tabia za kuwakatisha masomo mabinti waliopo mashuleni kuachana na Tabia hiyo kwani  imekuwa ikisababisha kudidimiza ndoto za wasichana wengi..






MBUNGE WA BUKOMBE AWATAKA WANANCHI KUVUNJA MAKUNDI YA VYAMA NA KUWA WAMOJA

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko akiwa kwenye Mkutano wa kutatua na kusikiliza Kero za wananchi kijiji cha Bwenda Kata ya Kantente.

Meza Kuuu hakiwepo Mbunge wa Jimbo la Bukombe pamoja na viongozi wa Kijiji cha Bwenda na wa kata ya Kantente.

Wananchi wakitoa kero zao mbele ya Mbunge wa Bukombe.






Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko akikabidhi mpira kwa Mwenyekiti wa Kijiji ambayo ilikuwa imeombwa na vijana kwaajili ya kujiandaa na Kombe la Dotto Cup
Diwani wa Kata ya Bulangwa Yusuf Mohamedi akielezea wananchi juu ya serikali ambavyo imejipanga kutatua Kero za wananchi juu ya Elimu pamoja na Huduma ya Afya.


Wananchi wa jimbo la Bukombe Mkoani Geita,wametakiwa kuachana na siasa ambazo  zinaweza kusababisha  kutokuwa wamoja katika kuleta maendeleo.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo  la hilo Dotto Biteko wakati akizungumza na wananakijiji wa kijiji cha Bwenda Namba 9 Kata Ya Kantente ambao ulikuwa na lengo la kusikiliza Kero za wananchi na kutatua changamoto walizo nazo.

Amesema kuwa maendeleo ya sehemu yoyote hile hayawezi kuletwa kwa watu kutokuwa na umoja na upendo.


"Wana Bwenda inahitajika nguvu ya pamoja ili kuhakikisha tuna maliza  changamoto za eneo letu, zikiwemo ukosefu wa miundo mbinu ya barabara, kituo cha Afya, miradi ya maji na kuzorota kwa ufaulu wa wanafunzi na niombe  wazazi mshirikiane  na walimu kwa kufuatilia kwa ukaribu zaidi maendeleo ya vijana mashuleni" Alisisitiza Dotto .

Hata hivyo ameongezea kuwa  kwa vijana wameanza kutenga  asilimia kumi ya mapato na tayari vikundi kumi vimekwisha kupatiwa Mkopo  na kwamba ameshapata fedha nyingine ambazo ni milioni hamsini na moja kwaajili ya maendeleo na mikopo kwa vijana na wanawake.

Pia amewataka wanakijiji hao kutokuwaogopa viongozi wao na 
kuwaambia kama wameshindwa kutekeleza majukumu yao ambayo waliyahaidi wakati wakiomba Ridhaa ya kuongoza kwani ni wajibu wao kuakikisha wanawatumikia wananchi ambao waliwaomba kura wakati wa kampeni.

.

Thursday 27 April 2017

WAWILI WATUMBULIWA NA WENGINE KUSIMAMISHWA KAZI KWAAJILI YA KUPISHA UCHUNGUZI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Elisha Lupuga akisoma maadhimio ya Baraza Juu ya kuwasimamisha Watumishi wawili ambao wamekiuka misingi  ya ajira.

Diwani wa Kata ya Nyamalimbe Jeremia Ikangala Akiunga Mkono maadhimio ya baraza la madiwani la kuwafukuza kazi watumishi na kuwasimamisha watumishi wengine kwaajili ya kupisha uchunguzi.

Baadhi ya madiwani wakifuatilia kikao maadhimio ya Baraza hilo.

Diwani wa Kata ya Nyarugusu Swalehe Juma akielezea juu ya hatua ambayo imechukuliwa kuwa ni mfano wa kuingwa kwa watendaji ambao wamekuwa na tabia za namna kutokutimiza majukumu ambayo wanatakiwa kuyafanya.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ,Ali Kidwaka akisikiliza maadhimio ambayo yalikuwa yakitolewa na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.


Baraza la Madiwani halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani humo kupitia mamlaka ya nidhamu ya watumishi imewafukuza kazi watumishi wawili wa halmashauri hiyo kwa utovu wa nidhamu na utoro kazini kwa muda mrefu. Na kuwasimamisha kazi watumishi wengine wawili kwa lengo la kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowakabili.

Akitanganza uamuzi huo mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Elisha Lupuga, baada ya baraza hilo kujiegeuza kuwa kamati ya nidhamu  kwa dharula  amesema hatua hiyo ni kuonesha namna gani watumishi wanatakiwa kufuata nidhamu kazini.

Mwenyekiti huyo amewataja waliofukuzwa kazi kuwa ni Nzalagaza Nyanda  ambaye alikuwa  idara ya utawala na Alphonce Mgimwa ambae alikuwa ni muuguzi katika zahanati ya  Furu ambae aliondoka kazini siku 50 bila taarifa .

Waliosimamishwa kwaajili ya uchunguzi ni mhandisi wa maji Halmashauri hiyo Rahel Antony ambae amesimamishwa kwaajili ya kupisha uchunguzi wa mradi wa maji wa Chankorongo ambao umesuasua kutokumalizika kwa miaka mingi na Denis Nyasaba ambae ni afisa ugavi wa halmashauri ambaye anachunguzwa kwa mikataba mibovu ya miradi.

“Kwa mujibu wa sheria za kanuni ya arobaini na mbili jedwali la kwanza sehemu A kipengele cha nne cha kanuni za utumishi wa uma  za mwaka 2003 na kanuni ya 57 kifungu kidogo cha kwanza  cha kanuni za utumishi wa uma ambapo namba F 16 kifungu kidogo cha kudumu cha mwaka 2009 watumishi hawa kuwa watoro kazini na kwamba wanaposhindwa kufika ofisini ndani ya siku tano sheria inatambua kuwafukuza kazi kwa hiyo natangaza kuanzia leo watumishi  hawa wamefukuzwa kazi kwa kuzingatia mamlaka ya kazi za uma “Alisisitiza Lupuga.

Madiwani wa Kataza Bukondo  na Lwamgasa John Maguru na Dotto Kaparatus amepongeza hatua hiyo huku wakiwataka watumishi kufuata kanuni na taratibu za mikataba ya ajira na pia kuwa waaminifu pindi wanapopatiwa  kazi.


IMEANDALIWA

Wednesday 26 April 2017

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA BUSINDA MKOANI GEITA AZUA TAHARUKI



Hofu  imetanda kwa wananchi wa kitongoji cha Sikalibuga kijiji cha Businda kata ya Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita kwa kuongozwa na wenyeviti wawili katika  kitongoji kimoja  kinyume na sheria.

Tuesday 25 April 2017

WAZIRI UMMY:TUWACHUKULIA HATUA WATAKAOTOZA FEDHA KUPIMA MALARIA NA KUUZA DAWA MSETO




Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa tamko kuhusu Siku ya Malaria Duniani kwa  waandishi wa Habari Mjini Dodoma na kusisitiza kuwa vipimo vya Malaria na Dawa za Mseto ni bure kwa vituo vyote vya Afya vya Umma nchini.



Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua Kitabu cha Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria katika kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi kutoka kamouni ya Gullin Pharma mara baada ya kuzindua Kitabu cha Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria katika kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali haitosita kuwachukulia hatua mtumishi yoyote katika vituo vya Afya vya Umma nchini watakaobanika kutoza fedha katika kutoa huduma ya vipimo vya malaria na kuuza dawa za Mseto kwa ajili ya kutibu ugonjwa huo.

Ameyasema hayo Mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa Habari kutoa tamko la Siku ya Malaria Duniani na kusisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kupata huduma ya kupima malaria pamoja na dawa za kutibu malaria bure katika vituo vya Afya vya Umma.

“Huduma ya kupima Malaria na dawa za Mseto zinatakiwa kutolewa bure katika vituo vyote vya Umma vya Huduma za Afya nchini na hatutosita kuwachukulia hatua watakaokiuka kutekeleza agizo hili.Alisistiza Mhe. Ummy.

Aidha amwewaagiza Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kutekeleza agizo hilo na kulisimamia kwa karibu ili kuondoa usufumbu kwa wananchi wanapotaka kupatiwa huduma hiyo.

Mhe Ummy Mwalimu amewashukuru wadau wote waliochangia kwa hali na mali katika mafanikio yaliyofikiwa ya mapambano ya dhidi ya Malaria nchini.

Siku ya Malaria Duniani uadhimishwa kila Aprili 25 ya kila mwaka na kwa mwaka huu kauli mbiu ni “ Shiriki kutokomeza Malaria kabisa kwa Manufaa ya Jamii”.



SERIKALI KUWEKEZA KWENYE VIFAA TIBA VITOKANAVYO NA PAMBA



Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unakamilisha taratibu za uwekeza kwenye vifaa tiba vitokanavyo na pamba na bidhaa za maji ya dripu(Infusion Fluids).

DC KAPUFI AWAHIMIZA MAAFISA KILIMO KUTOKUKAA OFISINI NA BADALA YAKE WAFANYE UTAFITI WA MAENEO YA KILIMO

Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Katandalo kata ya Kaseme juu ya kuhimiza kilimo ambacho kinastahili ukame wakati wa Ziara ya kutembelea mashamba ya pamba mtama na Mihogo.

Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwasili kwenye ofisi za Kijiji cha Katandalo.hapa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa kijiji hicho.


Mkuu wa wilaya akisaini kwenye kitabu cha wageni Kijiji cha Katandalo.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiwasisitiza wananchi kulima kilimo ambacho kitaleta manufaa kwao.




Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akikagua shamba la Mihogo 


Mkuu wa wilaya ya Geita akikagua shamba la pamba

Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimpongeza mkulima wa pamba ambaye alipendezwa na maendeleo ya shamba lake.


Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi amewataka maafisa kilimo na umwagiliaji kufanya tathmini halisi ya mazao  yanayoweza kustawi kwenye maeneo tofauti na mazao watakayobaini kuwa yanastawi vizuri wawahimize wananchi kuyalima

Mwl Kapufi amesema hayo wakati akiwa kwenye zoezi la kukagua mashamba ya pamba ,mtama na Mihogo kwenye Kata ya Kaseme na Magenge Wilayani Humo.

Amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya Hali ya Hewa ni vema maafisa kilimo wakatembelea maeneo na kuangalia  aina ya mazao yanayostawi

 “Kwa wilaya yetu ya Geita Halmashauri ya Wilaya na Halmashauri ya Mji natoa wito kwanza kwa maafisa kilimo na umwagiliaji wote waweze kufanya tathmini halisi ya mazao ambayo yanatakiwa kustawi katika eneo husika, hayo mazao ambayo yatastawi kwenye maeneo hayo ndiyo tuwahimize wananchi waweze kulima kwenye maeneo hayo”Alisema Kapufi.


Hata hivyo wakulima  wa zao la pamba katika kijiji cha Katangalo kata ya Kaseme wamemwambia Mkuu wa wilaya kuwa kukosekana kwa pampu za kutosha kwa ajili ya kunyunyuzia dawa kunasababisha uharibifu mkubwa  wa zao hilo la kibishara kwani kwa sasa wakulima takribani 300 wanatumia pampu moja ambayo haitoishi kwa mahitaji yao.


Akijibu kero hizo Mkuu wa Wilaya Mwalimu Herman Kapufi, amewataka watendaji wa serikali za  vitongoji na Vijiji kuwa na mfumo mzuri wa kubainisha changamoto za wakulima ili zipatiwe ufumbuzi.

Monday 24 April 2017

KOCHA WA TOTO ATAMBA KUFANYA VYEMA MECHI ZILIZOSALIA LIGI KUU.

Mfadhili wa timu ya Buselesele FC ,Godfrey Miti akifuatilia Mchezo wa TOTO na Buselesele FC ambapo ilikuwa ni mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye viwanja vya shule ya sekonadari ya Buselesele.

Mashambulizi yakiendelea kwa timu zote mbili.

Mashabiki wakifuatilia mtonange huo.




Benchi la Toto afrikani baadhi ya wachezaji wakicheki mchezo.






Kocha  Mkuu wa timu ya  Toto African ya Jijini Mwanza maarufu wanakisha mapanda,  Furgence Novatus amesema  timu hiyo kamwe  haitashuka daraja  kutokana na matumaini makubwa ya ushindi kwa mechi nne  walizobakiza licha ya kuwa wako katika mstali wa hatari kushuka ligi.

Kocha huyo ametoa tambo zake mara baada ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki kati ya Toto African na Buselesele FC, mabingwa wapya wa Mkoa wa Geita ligi daraja la tatu, ambapo Novatus amesema hata Mabingwa wa ligi kuu timu ya Yanga hawatawabakisha salama wasipojipanga na kwamba hakuna urafiki katika hatua waliopo.

Baada ya mchezo huo ambao timu hizo zilitoshana nguvu, wadau wa soka Mkoani Geita wamekuwa na matumaini makubwa na timu yao, ambayo iko katika maandalizi ya kuchuana ligi daraja la pili.

Diwani wa kata ya Buselesele Godfrey Miti ambaye ni mdhamini wa Timu ya Buselesele FC amedai kuwa matumaini makubwa aliyonayo ni kuakikisha timu hiyo inafikia kiwango cha ligi kuu na kwamba yeye pamoja na wadau wa mpira Mkoani Geita hataakikisha timu hiyo inapanda daraja.