Kamanda mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa geita Mponjoli Mwabulambo |
Wananchi mkoani Geita wameiomba serikali kudhibiti vitendo vya rushwa nchini
ambavyo vinapelekea kukosa haki zao za msingi wanapohitaji kuzipata.
Wakizungumza na Storm habari baadhi ya
wananchi hao ambao wamelishutumu jeshi
la polisi kwa kuendelea kujihusisha na vitendo hivyo ambavyo vimeonekana kuwabana zaidi wananchi wenye kipato
cha chini na kushindwa kupata haki zao.
Aidha kamanda wa polisi mkoa wa GeitaMponjoli
Lotson amekiri kuwepo kwa tuhuma
hizo huku akiwataka wananchi kuonyesha ushirikiano hasa kwa vielelezo ili wanaojihusisha na vitendo hivyo
wachukuliwe hatua za kisheria.
Kwa upande wake mkuu wa taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa (TAKUKURU) Bw.Thobias
Ndaro ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa katika ngazi husika pindi yatokeapo matukio hayo hali
itakayosaidia kuondoa tatizo hilo mkoani hapa.
No comments:
Post a Comment