Waziri wa nchi, ofisi ya rais, utumishi na utawala bora, Mh Angela Kairuki.
Wafanyakazi wa Taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa (takukuru),
wametakiwa kuanza kujisafisha huku wakiambiwa kwamba taasisi hiyo haitaepuka kutumbuliwa majipu.
Aidha, wameagizwa kuwasilisha upya taarifa
za mali zao kwa sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma, zifanyiwe uhakiki
wa mali; moja baada ya nyingine kubaini waliofanya udanganyifu wa umiliki wa
mali zao.
Waziri wa nchi, ofisi ya rais, utumishi na
utawala bora, Mh Angela Kairuki amesema
hayo jijini dar es salaam kwenye ufunguzi
wa mkutano wa mwaka wa viongozi wa taasisi hiyo.
Aidha amesisitiza kuwa tayari anazo
taarifa zinazohitaji baadhi ya viongozi wa taasisi hiyo kutumbuliwa majipu muda
muafaka utakapowadia.
Mh Kairuki ameagiza taasisi hiyo kufanyia tathmini
kesi zake zote, ilizowahi kushindwa na kuja na majibu ya sababu za kushindwa na
endapo itabainika hazikushinda kutokana na mchezo mchafu wa wachunguzi,
wahusika wachukuliwe hatua haraka iwezekanavyo.
Amesema iwapo yupo mtumishi hasa viongozi
wa taasisi hiyo, anayejitambua kuwa ni ‘jipu’, ajisalimishe kwani akiendelea
kusubiri na kutumbuliwa, mwisho wake
utakuwa mbaya.
No comments:
Post a Comment