Wakazi
wa mtaa wa stooni kata ya Ludete wilaya na mkoani Geita wamelalamikia suala la
kutaka kurudishwa kwa kiongozi wa serikali ya mtaa Bw.Aliphonce Masalakulangwa
aliekataliwa na wananchi kwa madai ya kukosa sifa ikiwa ni pamoja na kutumia
madaraka vibaya katika kipindi cha uongozi wake.
Wakizungumza
na storm habari wananchi hao wamedai kuwa hawamuhitaji kiongozi huyo arudi
katika uongozi huo kwani hata mwanzo amewahi kukataliwa kutokana na utendaji
wake kuwa mbovu.
Storm
habari imemtafuta Bw.Alphonce Masalakulangwa ili kuzungumzia jambo hilo ambapo
hakutaka kuzungumza kwa madai ya kwamba
hakuwa na maandalizi.
Kwa
upande wake kaimu mwenyekiti wa mtaa huo Bw.Ramadhani Mapera amekiri kuwepo kwa
tatizo hilo mtaani hapo huku akidai kuwa uongozi huo aliupata baada ya
mwenyekiti aliyekuwepo kukataliwa na wananchi na kwamba anashangazwa na hatua
ya mtendaji wa kata hiyo kutengua uamuzi huo.
Aidha
storm habari ilifanya jitihada za kuwatafuta Afisa mtendaji wa kata hiyo
Bi.Josephina Mgaya pamoja na diwani wake lakini jitihada hizo ziligonga mwamba
kwani hawakutaka kuzungumza wakidai kuwa
na majukumu mengi.
No comments:
Post a Comment