Leo ni siku ya maji duniani inayoadhimishwa kila siku ya tarehe 22
mwezi wa tatu kila mwaka duniani, Katika siku ya leo kauli mbiu ikiwa ni
KUPUNGUZA IDADI YA VIFO VITOKANAVYO NA UPUNGUFU WA MAJI MWILINI KWA KUHAKIKISHA
MATUMIZI YA MAJI SAFI NA SALAMA.
Shirika la afya duniani(WHO) limetoa ripoti kuwa katika kila
dakika mbili mtoto mmoja hukabiliwa na athari ya kufariki dunia kutokana na
kunywa maji machafu pia katika hatua nyingine asilimia 10 ya watu duniani
hawapati maji safi ya kunywa na kwa msingi huo wanakabiliwa na hatari ya
maradhi ya tumbo na kufariki dunia.
Wakatib huo huo pia shirika la watoto duniani(UNICEF)
limetahadharisha kutokuwepo maendeleo ya kutoshakatika suala la kudhibiti maji
taka inapelekea maisha ya watoto yakabiliwe moja kwa moja na hatari kubwa na
kupoteza maisha.
No comments:
Post a Comment