Thursday 29 September 2016

UINGEREZA YACHANGIA BILIONI 6 KWA AJILI YA UKARABATI WA SHULE MKOANI KAGERA


Uingereza imetoa mchango wa Shilingi Bilioni 6 kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa miundombinu ya shule zilizopata madhara kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea katika Mkoa wa Kagera tarehe 10 Septemba, 2016.

Wednesday 28 September 2016

SPIKA MSTAAFU SAMWELI SITTA APELEKWA UJERUMANI KUTIBIWA


Hali ya Afya ya Spika mstaafu, Samuel Sitta si nzuri,baada ya Serikali kumpeleka nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA KOREA YA KUSINI


Waziri mkuu Kassim Majaliwa amekutana na wawekezaji wa kampuni tisa za nchini Korea Kusini  na kumuahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuwekeza katika sekta ya kilimo, viwanda, maji, miundombinu, elimu, afya na michezo.

Tuesday 27 September 2016

BARAZA KUU LA UONGOZI CUF LAMFUTA UANACHAMA PROFESA LIPUMBA

Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) Taifa lililokutana Zanzibar leo limemfukuza uanachama Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba.

BABA AJINYONGA BAADA YA KUMPIGA BINTI YAKE HADI KUPOTEZA MAISHA MKOANI GEITA



Mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Martha Charles Mwenye umri wa miaka 15 ameuwawa kwa kupigwa  na fimbo na Baba yake mzazi kisha baba yake aliyefahamika kwa jina la Charles Mlima  kujinyonga baada ya tukio hilo lilitokea  katika kata na kijiji cha kaseme wilayani na Mkoani Geita.


Akizungumza na Stormfm ndugu wa familia hiyo John Lufunguro  amesema  kuwa marehemu ambae ni mtoto wa Baba huyo alikumbwa na mauti hayo  baada ya kupigwa na baba yake kwa kile kilichodaiwa kuwa  amekutwa katika hali ya kimapenzi, hali ambayo haikumpendeza baba yake kutokana na kuwa na umri mdogo kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi.

NDEGE YA PILI YA BOMBARDIER Q-400 YAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM LEO, RAIS MAGUFULI KUZIZINDUA NDEGE HIZO KESHO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kesho anatarajiwa kuzindua ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q 400 zilizonunuliwa na Serikali hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Kesho kuanzia saa mbili asubuhi.

“Tunawaomba wanahabari na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji wa ahadi wa Serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa Anga hapa nchini”, amesema Dkt. Chamuriho.

Ndege hizo aina ya Bombardier Q 400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja  zimetengenezwa nchini Canada na zitahudumia soko la ndani ndani na nchi za jirani zitakapoanza kazi.


Katibu Mkuu Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamriho akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi pamoja na maafisa wengine wakiwa katika Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.


Katibu Mkuu Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamriho na viongozi wengine wakielekea kwenye Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ilipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba



RAIS MAGUFULI AANZA KUWASHUGHULIKIA WANAOHUJUMU MISAADA KAGERA













Leo September 27 2016 taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa muda mfupi baada ya kupokea hundi ya msaada wa Milioni 545 kutoka kwa Waziri Mkuu wa India imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Steven Makonda.

Monday 26 September 2016

ALIYOAGIZA LEO RAIS MAGUFULI BAADA YA KUFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI JIJINI DSM

Leo September 26 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametembelea Bandari ya Dar es Salaam na kuzungumza na wafanyakazi wa bandari hiyo ambapo pamoja na mambo mengine ametoa miezi miwili kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kununua mashine nne za kukagulia mizigo bandarini (Scanning Mashine).

MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI YAMEZINDULIWA RASMI LEO MKOANI GEITA



naibu waziri wa mambo ya ndani Mhandisi Hamad Masauni azindua wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani, Kitaifa Mjini Geita leo


Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiyaangalia maandamano ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.


Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Mohamed Mpinga akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani.

Washiriki wa maonyesho (waendesha bodaboda) wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani mjini Geita leo.

Maadhimisho  ya  Wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani yamezinduliwa Rasmi leo Mkoani Geita katika viwanja vya Kalangalala  na Naibu Waziri wa mambo ndani Mh.Ahamed Masauni, huku ajali za waendesha piki piki maarufu  boda boda zikiendelea kushika kasi kubwa  zaidi nchini.

AFISA UVUVI NA MRATIBU ELIMU WAWEKWA CHINI YA ULINZI KWA MADAI YA KUTETEA UVUVI HARAMU

Afisa Uvuvi kata ya Nkome Merina Damian na Mratibu Elimu Kata Thom Sharusanga wamewekwa chini ya ulinzi na Mkuu wa Wilaya ya Geita Herman Kapufi baada ya kudaiwa kuhusika kuwatetea wavuvi haramu ambao wamekuwa wakijihusisha kuvua samaki ambao hawaruhusiwa kwa kutumia nyavu haramu za dududuu.

Hatua ya kusimamishwa imekuja baada ya Mwenyekiti wa kitongoji Simon Kinasa kuanzisha operesheni na kuwakamata baadhi ya watu wanaovua samaki chini ya kiwango ambapo baada ya kuwakamata afisa uvuvi na Mratibu wakamuamuru awaachie wakidai mwenyekiti amewakamata kwa madai amenyimwa rushwa.

Friday 23 September 2016

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI YA BUKOMBE MKOANI GEITA YAMHUKUMU MWALIMU KWA KOSA LA KUOMBA RUSHWA













Mahakama  ya Hakimu Mkazi ya Bukombe mkoani Geita imemhukumu Mwalimu wa Shule ya Msingi Umoja, Daniel Nyingati kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh milioni 1.6 baada ya kupatikana na makosa ya  kuomba na kupokea rushwa.

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATUNUKIWA TUZO YA UONGOZI WA KISIASA NA UTETEZI


Shirika lisilo la  Kiserikali la Speak  Up for Afrika    limemtunukia tuzo, Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kutokana na uongozi wake wa kisiasa na utetezi wake  kwa  makundi ya jamii yaliyo katika mazingira magumu hususani wanawake na watoto.

FAHAMU MECHI ATAKAZOZIKOSA LIONEL MESSI BAADA YA KUPATA JERAHA KATIKA MGUU WAKE(GROIN)


Usiku wa Septemba 21 Ligi Kuu Hispania iliendelea kama kawaida kwa michezo kadhaa kupigwa, lakini moja kati ya michezo iliyochezwa ni pamoja na mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Atletico Madrid uliomalizika kwa sare ya goli 1-1.

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE LEO SEPTEMBER 23

Kufuatia hatua ya Serikali kununua hisa zote za Bharti Airtel ambaye alikuwa mbia mwenza wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na hivyo Serikali kumiliki hisa za Kampuni hiyo kwa asilimia 100, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Waziri Waziri Kindamba kuwa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.

Waziri Waziri Kindamba ameteuliwa kushika nafasi hiyo kuanzia leo September 23 2016. Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura atapangiwa kazi nyingine.

Thursday 22 September 2016

MAJINA YA WALIOFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA BASI LA SUPER SHEM JIJINI MWANZA






































Watu 13 wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la Super Shem lenye namba za usajili T 874 CWE lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Mwanza na Hiace yenye namba T 368 CWQ iliyokuwa ikitoka Jijini Mwanza kuelekea Wilaya ya Kwimba.

Wednesday 21 September 2016

RAIS WA BOTSWANA AMTAKA ROBERT MUGABE AJIUZULU



Rais wa Botswana kushoto Ian Khama na mwenzake wa Zimbabwe Robert Mugabe

M-PAWA KUTOKA VODACOM YAZIDI KUWATAJIRISHA WATANZANIA MSHINDI WA PILI APATIKANA



 Meneja masoko Huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania ,Noel Mazoya (katikati) akiongea na mmoja wa mshindi wa droo ya promosheni ya Jiongeza na M-Pawa wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkazi wa Arusha Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Meneja wa Huduma za M-Pawa wa Benki ya CBA Eric Luyangi na Msimamizi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini Bakari Maggid

RAIS MAGUFULI AIPONGEZA KILIMANJARO QUEENS KWA UBINGWA WA CECAFA CHALENJI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewapongeza wachezaji wa Timu ya soka ya Wanawake ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Queens) kwa kuandika historia ya kuwa Mabingwa wa kwanza wa Michuano ya kugombea kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge) iliyofanyika katika Mji wa Jinja nchini Uganda.

WAZIRI NAPE NNAUYE AIPONGEZA KILIMANJARO QUEENS MABINGWA KOMBE LA CECAFA




Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewapongeza Wachezaji wa Kilimanjaro Queens kwa niaba ya serikali na kwa niaba ya watanzania kwa kazi nzuri waliyoifanya mpaka kuwa mabingwa wa kwanza wa Kombe la CECAFA kwa mpira wa miguu kwa wanawake Afrika Mashariki na Kati.

PICHA:MKUU WA MKOA WA KAGERA AIPOKEA KILIMANJARO QUEENS. AWAPONGEZA KWA USHINDI






Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa Kilimanjaro mara baada ya kuwasilini Mkoani Kagera wakitokea nchini Uganda kushiriki mashindano ya CECAFA kwa wanawake ambapo wameibuka mabingwa kwa mwaka 2016.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu akipokea kikombe cha ubingwa wa CECAFA kwa wanawake kutoka kwa Nahodha wa Kilimanjaro Queens Sophia Mwasikili.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu(kushoto) akiinua juu kikombe cha ubingwa wa CECAFA kwa wanawake alichokipokea kutoka kwa Nahodha wa Kilimanjaro Queens Sophia Mwasikili(kulia).



Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Kijuu(kushoto) akipokea Bendera ya Taifa kutoka kwa katibu wa Chama cha Mpira mkoani Kagera Bw. Salum Chama mara baada ya Mabingwa wa CECAFA kwa wanawake Kilimanjaro Queens kuwasili kutoka Nchini Uganda katikati ni Mwenyekiti wa Soka la wanawake Amina Karuma.

WATU WENGINE KADHAA WAUAWA KATIKA MAANDAMANO NCHINI CONGO DRC



Waandamanaji nchini Congo DRC

Watu wengine kadhaa wameuawa katika siku ya pili ya machafuko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana, huku makao makuu ya vyama vitatu vya upinzani yakichomwa moto.
Hayo yamejiri katika wimbi jipya la makabiliano kati ya polisi na wapinzani wa Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila 

PICHA: BASI LA SUPER SHEM LAPATA AJALI NA KUUA WATU 11 JIJINI MWANZA HII LEO






Basi la Super Shem linalofanya safari za Mwanza kwenda  Mbeya limepata ajari ya kugongana na hiace katika kijiji cha Hungumalwa Mwanza na kusababisha vifo vya watu  wanaodaiwa kufika 11 asubuhi hii.

Tuesday 20 September 2016

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA WAATHIRIKA WA AJALI MKOANI NJOMBE



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizopatwa na msiba kufuatia ajali ya basi la kampuni ya New Force iliyotokea jana Sept 19, 2016 majira  ya saa 2:00 usiku katika kijiji cha Lilombwi, kata ya Kifanya mkoani Njombe. 

UTEUZI MWINGINE WA RAIS MAGUFULI LEO SEPTEMBER 20 2016



Leo September 20 2016 taarifa iliyotolewa Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania. 

WAZIRI MKUU APOKEA MCHANGO WA WATUMISHI WA SERIKALI WA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amepokea jumla ya sh. bilioni 1.040 kutoka kwa watumishi na wadau mbalimbali zikiwa ni misaada kwa wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu.

TIMU YA SOKA YA WANAWAKE(KILIMANJARO QEENS) WATWAA KOMBE LA CECAFA CHALLENGE



Timu ya soka ya wanawake ya Tanzania Bara (The Kilimanjaro Qeens) imetwaa kombe la Challenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, baada ya kuifunga Kenya, mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliopigwa leo Jinja , nchini Uganda.
Kwa matokeo hayo, Kilimanjaro Qeens wanakuwa ndiyo mabingwa wa kwanza na wa kihistoria wa michuano hiyo ambayo ni mipya kabisa kuanzishwa katika ukanda ukanda wa Afrika Mashariki chini ya baraza lake la CECAFA.

PICHA:SERIKALI KUSAMBAZA CHAKULA SALAMA KWA WAATHIRIKA WA SUMUKUVU



PICHA:MOJA YA NDEGE MPYA ZA ATCL ZILIZONUNULIWA NA SERIKALI YAWASILI NCHINI HII LEO



Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.


Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakisubiri kuwasili kwa Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016







Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikipata saluti ya maji (Water Canon Salutation) toka kwa magari ya Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mara tu bada ya kuwasili  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016





Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akisalimiana na Rubani aliyerusha Ndege mpya moja kati ya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.




Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakiwa kwenye  Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016







Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akipeana mikono kwa furaha na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu mara baada ya  Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016, Wengine ni marubani wa ndege hiyo