Kifua Kikuu (TB) ni ugonjwa ambao unafahamka kwa
watu wengi katika Tanzania kutokana na madhara mengi ambayo yamejitokeza
na kuonekana iwe katika familia au katika jamii kwa namna moja au nyingine.
Huu, ni ugonjwa ambao umedumu kwa karne nyingi
tangu ulipogunduliwa na mtaalam kutoka Ujerumani, Dk Robert Koch mwaka 1882 na
kuushangaza ulimwengu wa tiba kwa ugunduzi wake huo.
Mgunduzi wa Kifua Kikuu, Robert Koch
alipewa tuzo ya amani ya Nobel kwa ugunduzi wake huu ambao kwa kiasi kikubwa
umeiokoa dunia.
Kwa nyakati tofauti, walimwengu wakiwamo wanasayansi walikaa na kukubaliana kuanzisha Siku ya Kifua Kikuu duniani itayoadhimishwa kila siku ya Machi 24 kila mwaka.
Siku hiyo ni mahsusi kwa ajili ya kufanya mapitio kuhusu hali halisi ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Kwa hiyo, siku hiyo ya ugunduzi wa Dk Koch hadi
sasa imekuwa ikiadhimishwa kote duniani kila mwaka na kwa mwaka huu ikiwa
na kauli mbiu, ‘Tuungane kutokomeza Kifua kikuu`
Inaelezwa kuwa mtu menye vijidudu vya ugonjwa huo
akihoa, kupiga chafya au kwa namna yoyote nyingine kurusha vitone vya makohozi
yake kutoka katika mfumo wake wa hewa na kuvieneza hewani na mtu mwingine
kumpata akivuta hewa ndani na hivyo kuingia katika mfumo wa hewa.
Ugonjwa wa kifua kikuu ni kati ya magonjwa matatu
yanayotokea kwa kiasi kikubwa na kuwapata watu masikini zaidi .
Vifo vinavyotokana na ugonjwa wa kifua kikuu ni
32,000 kila mwaka katika Tanzania.
Kulingana na WHO, Tanzania ni ya 15 kati ya nchi 22 ambazo zimeathiriwa na ugonjwa huu barani Afrika.
Kulingana na WHO, Tanzania ni ya 15 kati ya nchi 22 ambazo zimeathiriwa na ugonjwa huu barani Afrika.
Kati ya asilimia 50 ya wagonjwa wa Kifua Kikuu
waliopimwa virusi vya Ukimwi mwaka 2007, inakadiriwa kuwa asilimia 47 walikuwa
pia na virusi vya Ukimwi.
Ugonjwa huu husababishwa na bakteria
waitwao, Mycobacteria tuberculosis.
Aina hii ya bakteria huathiri mapafu, tezi (lymph
nodes), tumbo na sehemu nyingine za mwili.
Wataalam wanaeleza kuwa asilimia 10 tu ya watu walio na bakteria hao jamii ya Mycobacteria tuberculosis hawapati ugonjwa huu wa Kifua Kikuu.
Wataalam wanaeleza kuwa asilimia 10 tu ya watu walio na bakteria hao jamii ya Mycobacteria tuberculosis hawapati ugonjwa huu wa Kifua Kikuu.
Ø Aina za Kifua Kikuu
Kuna aina kuu tatu za ugonjwa wa Kifua Kikuu;
-Kifua kikuu kinachosababisha madhara (active tuberculosis) – hutokea pale ambapo bakteria waliopo mwilini wapo hai na kinga ya mwili imeshindwa kuwadhibiti hawa bakteria wasisababishe madhara. Watu hawa wanaweza kumuambukiza mtu yoyote kifua kikuu kwa njia ya kuvuta pumzi kama watakohoa, kutema mate, kupiga chafya, kupiga kelele iwapo watafanya vitendo hivi karibu na watu wasio na ugonjwa huu.

-Ugonjwa
usiosababisha madhara (inactive tuberculosis) – Kwa kitaalamu huu pia
huitwa Latent TB. Hapa inaamaanisha kuwa kinga ya mwili imeweza kuwadhibiti
bakteria na kuwafanya kushindwa kusababisha madhara.
Mtu mwenye Latent TB, hana dalili za ugonjwa huu,
hajisikii mgonjwa na hawezi kuambukiza mtu mwingine ugonjwa wa kifua kikuu.
Aina hii inaweza kujirudia baadaye na kuathri
sehemu ya juu ya mapafu na hivyo kusababisha kikohozi cha kawaida ambacho
baadaye huongezeka na kusababisha kikohozi cha damu au makohozi, homa, kupungua
hamu ya kula, kupungua uzito bila sababu ya msingi na kutokwa jasho kwa wingi
kuliko kawaida wakati wa usiku.
-Ugonjwa
uliosambaa mwilini (milliary tuberculosis) – Hii hutokea pale ambapo kinga
ya mwili imepungua na kusababisha ugonjwa wa kifua kikuu kuenea kupitia damu
hadi sehemu nyingine za mwili kama mifupa, mishipa ya fahamu, ngozi, figo,
kibofu cha mkojo, ngozi ya moyo (pericadium), mfumo wa uzazi, viunganishi vya
mifupa (joints) na lymphatic system.
Husababisha homa, kupungua hamu ya kula, kuchoka
na kupungua uzito.
Vihatarishi vya ugonjwa wa Kifua Kikuu
Vihatarishi vya ugonjwa wa Kifua Kikuu
Ø Vihatarishi vya ugonjwa huu ni;
-Uzee
-Unywaji pombe kupindukia
-Kuishi sehemu zilizo na mrundikano wa watu kama mabweni, kambi za jeshi, hospitali, mabasi ya abiria.
-Magonjwa yanayoathiri kinga ya mwili kama Kisukari.
-Wafanyakazi wa huduma ya afya
-Ugonjwa wa Ukimwi
-Utapiamlo
-Umaskini au hali duni ya kipato
-Kuishi kwenye nyumba za jamii, mfano nyumba za wazee
-Wale wasio na makazi
-Baadhi ya dawa – Dawa za ugonjwa wa maumivu ya mifupa (athritis)
-Wasafiri au watalii kutoka nchi zilizo na idadi kubwa ya ugonjwa wa kifua kikuu.

Ø Dalili na viashiria vya ugonjwa wa Kifua Kikuu
-Kukohoa zaidi ya wiki 2-3 na kuongezeka kutoa makohozi
-Kukohoa damu
-Homa za mara kwa mara
-Kupungua au kukosa hamu ya kula
-Kupungua uzito kwa asilimia 10.
-Kutokwa na jasho kwa wingi hasa wakati wa usiku
-Uchovu
-Maumivu makali ya kichwa
-Maumivu ya kifua
-Kupumua kwa shida
Vipimo vya Kifua Kikuu
-Kipimo cha makohozi (Sputum for AFB) – Makohozi huchukuliwa kwa siku tatu mfululizo muda wa asubuhi na kupelekwa maabara kufanyiwa uchunguzi ili kuweza kugundua kama mtu ana TB.

Kwa wale wagonjwa wasioweza kutoa makohozi au
wale wenye TB ya tumbo, basi hufanyiwa kipimo cha gastric lava.
KWA PAMOJA TUUNGANE KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU. 8
No comments:
Post a Comment