Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (Mb) akipokea
Mwenge wa Uhuru baada ya kuwasili kwenye jimbo lake la Muhambwe Wilayani
Kibondo mkoani Kigoma.
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto)
akishiriki uzinduzi wa Kituo cha Afya cha Mabamba kilichopo kwenye jimbo lake
la Muhambwe wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru za kitaifa uliofanyiwa na
kiongozi wa kitaifa wa mbio hizo Bwana Charles Kabeho (wa tatu kushoto) kwenye
kata ya Mabamba wilayani Kibondo, Kigoma
Mkuu
wa Wilaya ya Kibondo Mheshimiwa Loyce Bura (kulia) akipokea mbio za Mwenge wa
Uhuru wa Taifa kwenye kijiji cha Mkubwa kilichopo mpakani mwa Wilaya ya Kibondo
na Kakonko
Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akigawa chandarua
kwa wanawake wenye watoto baada ya uzinduzi wa kituo cha Afya cha Mabamba
kilichopo kwenye jimbo lake la Muhambwe wilayani Kibondo, Kigoma wakati wa mbio
za Mwenge wa uhuru za kitaifa
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Atashasta Nditiye, Mbunge wa jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo, Kigoma akipiga
ngoma kuburudisha wapiga kura wake wakati wa kupokea mbio za Mwenge wa Uhuru za
kitaifa uliowasili kwenye Wilaya hiyo
Hayo yameelezwa na Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (Mb) wakati
akipokea mbio za mwenge wa Uhuru ulipowasili Wilaya ya Kibondo kwenye jimbo
lake la Muhambwe ukitokea Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma. Amesema kuwa Wilaya
ya Kibondo imeongoza kwa ufaulu wa shule za sekondari kwa miaka miwili
mfululizo ya masomo mwaka 2016 na 2017 ambapo kidato cha pili wameshika nafasi
ya nane kitaifa na kidato cha nne wameshika nafasi ya tisa kitaifa na kuzibwaga
sekondari nyingine zilizopo kwenye jumla ya Wilaya 187 nchini.
Nditiye amefafanua kuwa
shule hizo zimezawadiwa kiasi cha shilingi milioni 680 na Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia kupitia Mpango wa Elimu kwa Matokeo (E4P) ambao umeleta
chachu, ari na ushindani kwenye kiwango cha ufaulu kwenye shule mbalimbali
nchini. Amefafanua kuwa fedha hizo zimetumika kugharamia upatikanaji wa
miundombinu mbalimbali kwenye shule ya sekondari ya Malagarasi na ya Wasichana
ya Kibondo.
Ameongeza kuwa ushindi
huo umeleta chachu na mwamko zaidi kwa wanafunzi, walimu, wazazi, walezi na
wadau wa elimu kwenye Wilaya hiyo ambapo wamejipanga kuchangia ujenzi wa
miundombinu mbali mbali kwenye shule za Wilaya hiyo ili kuongeza ufaulu kwa
wanafunzi ambapo imeendana na kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu
isemayo, “Elimu ni Ufunguo wa Maisha, Wekeza Sasa kwenye Elimu kwa Maendeleo ya
Taifa”.
Mhandisi Nditiye amesema
kuwa Wilaya ya Kibondo inaunga mkono jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muunano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli za kutoa elimu bure nchini kote
kwa shule za msingi na sekondari ambapo wazazi hawalipi ada yeyote hivyo
inawawezesha kushirikiana kuendeleza miundombinu ya shule na mahitaji ya huduma
nyingine ili wanafunzi waweze kujisomea na hivyo kuongeza ufaulu wao.
Naye kiongozi wa kitaifa
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu Bwana Charles Kabeho amewataka wazazi
na walezi kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha kuwa wanamuunga mkono Mhe. Rais
wa nchini yetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata
sare za shule, vitabu vya masomo mbali mbali na miundombinu mingine ili
kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa manufaa ya wanafunzi na
walimu.
Amefafanua kuwa azma ya
Dkt. Magufuli ni kuwa na nchi ya viwanda na kufikia uchumi wa kati ambapo haya
yote hayawezekani pasipo kuwa na taifa lenye rasilimali watu yenye elimu, ujuzi
na maarifa ya kuendesha na kusimamia viwanda vyetu.
Bwana Kabeho amemshukuru
na kumpongeza Mhandisi Nditiye kwa kutambua umuhimu wa mbio za Mwenge wa Uhuru
kitaifa na kujumuika na wananchi wa jimbo lake la Muhambwe lililopo kwenye
Wilaya ya Kibondo. “Mheshimiwa Nditiye, natambua majukumu uliyonayo katika
kipindi hiki cha Bunge la bajeti ambalo linaendelea mkoani Dodoma lakini
umejali na kuja kujumuika nasi katika kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo
kwenye Wilaya hii,” amesema Kabeho.
Mbio za Mwenge wa Uhuru
kitaifa zimepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mheshimiwa Loyce Bura kwenye
kijiji cha Mkubwa mpakani mwa Wilaya ya Kibondo ukitokea kwenye Wilaya ya
Kakonko. Mwenge umetembezwa kwenye Wilaya ya Kibondo na kuzindua miradi mbali
mbali ya maendeleo yenye jumla ya thamani ya shilingi 1,512,000,000 ikiwemo
kituo cha Afya cha Mabamba, kiwanda cha kusindika na kuzalisha unga wa muhogo,
ofisi ya ushauri wa kibiashara, hoteli na kugawa asiimia kumi ya mapato ya
Halmashauri hiyo kwa vikundi vya wajasiriamali wanawake, vijana na walemavu
kiasi cha shilingi milioni 58.
Mwenge umekabidhiwa
kwenye Wilaya ya Kasulu ili kuendelea na mbio zake na kuzindua miradi mbali
mbali ya maendeleo nchini ambapo makabidhiano hayo yamefanyika kwenye kijiji
cha Mvugwe mpakani mwa Wilaya ya Kibondo na Kasulu.
No comments:
Post a Comment