Kamanda mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Geita , Mponjoli Mwabulambo |
Agizo la Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John
Pombe Magufuli la kupiga marufuku kucheza Pool nyakati za
kazi limeanza kutekelezwa mkoani Geita katika Wilaya ya Bukombe na
kwamba Jeshi la Polisi limewanasa na kuwatia mbaroni vijana 22
wakicheza mchezo huo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita kamishna msaidizi
Mponjoli Mwabulambo amesema vijana hao walikamatwa jana katika msako mkali
unaoendelea na kufikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Mponjoli amesema msako huo umelenga maeneo ya Stend za
magari mjini ushirombo pamoja na kwenye nyumba za starehe
yaani Bar na maeneo mengine ambayo huchezwa mchezo huo
ambao serikali imeupiga marufuku kuchezwa nyakati za kazi.
Mwanzoni mwa wiki hii Rais Magufuli wakati akiwaapisha
wakuu wa Mikoa nchini alipiga marufuku mchezo wa Pool na kuwaagiza viongozi hao
mikoani kuhakikisha wanawakamata wale wote watakaobainika wanacheza Pool wakati
wa Kazi na sasa mchezo huo utachezwa kuanzia saa 10 jioni.
Aidha Mponjoli amesema msako huo utaendelea katika maeneo
yote ya wilaya ya Bukombe ikiwemo kwenye miji yote yenye mikusanyiko ya watu
hata vijiji ambako mchezo huo unachezwa nyakati za kazi hali itayofanya Agizo
la Rais Magufuli la kila mtu kufanya kazi linatekelezwa .
Pia Mponjoli amewaonya vijana wote wanaojihusisha na
Uharifu wa aina yoyote waache mara moja kabla ya kukamatwa kwani shughuli ya
wizi huo katika awamu hii ya Tano haina nafasi na kuwataka wakafanye kazi
zingine ambazo ni halali za kuwaingizia kipato.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Polisi Wilaya ya Bukombe SP
Leonard Nyandahu amesema wafanyabiashara wote wanaomiliki Pool katika miji ya
Ushirombo na Runzewe,Uyovu wameziondoa Pool zote kwenye maeneo yao yote ya
biashara zao.
Nyandahu amesema kuwa katika msako wake wafanya
biashara hao wengi wao wamefunga kabisa mchezo wa Pool kwenye maeneo yao ya
Biashara kwa madai kuwa wanamuunga mkono Rais Magufuli ambaye katika agizo lake
alisema mchezo huo uchezwe kuanzia saa 10 jioni lakini wao wamefuta kabisa
katika maeneo yao kwani vibaka walikuwa wakitumia kufanya mipango yao ya
uharifu.
No comments:
Post a Comment