Thursday 31 May 2018

WATU ZAIDI YA MILIONI 7 WANAFARIKI KWA MATUMIZI YA SIGARA


Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema uvutaji wa sigara unabaki kuwa chanzo kikuu cha vifo ambavyo vingeepukika licha ya kupungua kwa matumizi ya sigara duniani tangu kuanza kwa karne ya 21. 

"WIZARA, TAASISI ZA SERIKALI ZITUMIE NISHATI MBADALA" – PM MAJALIWA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuzindua Maadhisho ya Wiki ya Mazingira, Mei 31, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.  


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es salaam, Kate Kamba wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam kuzindua Wiki ya Mazingira, Mei 31, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla na watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani , Mhandisi Evarest Ndikilo. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Space Engineering Limited, Bw. Philip Mtui kuhusu mkaa uliotengenezwa kutokana na takataka na kufungashwa kwenye kiroba tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. katikati ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarest Ndikilo. 



 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji  wa Kampuni ya  Space Engineering Limited, Bw. Philip Mtui kuhusu  mkaa uliotengenezwa kutoka na takataka na kufungashwa kwenye kiroba tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea banda la Kampuni hiyo kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarest Ndikilo na kushoto ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Neema Matemba. 



 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Edosama Hardware Limited, Edward Maduhu kuhusu bidhaa mbalimbali zinazotokana na miti ambazo zinatengenezwa na kampuni hiyo wakati alipotembelea mabada ya maonyesho kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Mei 31, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi Nimwagile Mwaijumba wakati alipotembelea banda la Kituo cha Utengenezaji magari cha Nyumbu  na kujionea mashine ya kutengeneza mkaa bora kwa kutumia takataka iliyobuniwa na kutengenezwa na kituo hicho. Waziri Mkuu alitembelea mabanda ya maonyesho  kabla ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Opwani Mhandisi, Evarest Ndikilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya JHS , David Mwendapole  wakati alipotoa maelezo kuhusu majiko makubwa yanayotumia  gesi kidogo  katika maonyesho ya Wiki ya Mazingira kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. Wanne kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba. 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Mei 31, 2018. 

Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 31, 2018. 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi baada ya kuzindua Wiki ya Mazingira kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangala, Mwenyekiti wa CC wa Mkoa wa Dar es alaam, Kate Kamba,Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori  na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba. 

SERIKALI KUENDELEA KUCHUKUA HATUA ZA KISERA KUHAKIKISHA RIBA ZA MIKOPO ZINAPUNGUA


Waziri wa Madini Mhe. Angellah   Kairuki akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka 2018/2019 leo Bungeni  Jijini Dodoma.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Uratibu  Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo  Bungeni kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali katika kuwalinda watoto wa kike ambapo ameahidi kuwa Serikali itatoa taarifa rasmi kuhusu kuwepo kwa baadhi ya watu wanaowadhalilisha kijinsia watoto wa kike  na hatua zilizochukuliwa na Serikali.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kupambana na Janga la Ukimwi hapa nchini ikiwemo kuhamasisha upimaji wa Virusi vya UKIMWI  hasa kwa wanaume kote nchini ili wajue hali zao na kuchukua hatua stahiki.


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo (wakwanza kushoto) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Mhe Angellah Kairuki Bungeni Jijini Dodoma leo.


Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa Kikula aliyesimama (kushoto) na Mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo Prof. Abdulkarim Mruma wakitambulishwa Bungeni leo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Sehemu ya Viongozi wa Tume ya Madini na wageni  mbalimbali wakiwemo wakuu wa Mikoa yenye madini wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Bungeni Jijini Dodoma leo.

 
 Sehemu ya Wanafunzi waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

Tuesday 29 May 2018

WAZAZI WATAKIWA KUACHA KUWAAGIZA WATOTO MAENEO YA MGODI WA GGM


Watoto wakiwa kwenye shimo la kutupia uchafu ndani ya mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM)wakiogota vyuma chakavu vinavyokuwa vimetupwa na mgodi huo.




Afisa mahusiano wa mgodi wa GGM Mussa Shunashu akionesha maeneo ambayo ni hatarishi kwenye mgodi huo.


Eneo la kutupia taka kwenye mgodi wa dhahabu wa Geita.


Bi. Sarah Kajoro akiwa kwenye masikitiko kutokana na mtoto wake kushindikana na kujikuta akielekea maeneo ya mgodini.


Mzazi akijaribu kumwazibu mwanae kutokana na kuwa na tabia ya kwenda kwenye maeneo ya mgodi wa GGM.


Mwenyekiti wa mtaa wa Kompaundi Edgha Onyango akielezea hatua ambazo wameendelea kuzichukua dhidi ya wazazi ambao wamekuwa wakiwaruhusu watoto wao kwenda maeneo ya mgodini.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl. Herman Kapufi akikemea vikali tabia ya baadhi ya wazazi kuendelea kuwatumikisha watoto kuwa watafutaji badala ya wao kutafuta.

WAVUVI KATA YA NKOME WALALAMIKIA KUONEWA NA WATU KUTOKA IDARA YA UVUVI


Wavuvi wa mwalo wa Makatani kata ya Nkome  wilayani Geita wakiendelea na maandalizi kwaajili ya kwenda kwenye shughuli ya uvuaji wa dagaa.


Zana za uvuvi ambazo wamelalamikiwa kuwa zinakamatwa na maafisa uvuvi kwa madai kuwa zinashiriki kwenye suala la uvuvi haramu.

Mzee Yohana Kulwa akielezea masikitiko yake kutokana na suala kuendelea kukamatwa na kupigwa faini na watu wa idara ya uvuvi bila ya kuwa na makosa yoyote.


Wavuvi wa Mwalo wa makatani Kata ya nkome Wilaya na Mkoa wa Geita,wamelalamikia kuonewa na watu kutoka idara ya uvuvi kutokana na kuendelea kuwakamata na kuwapiga faini pasipokuwa na makosa yoyote hali ambayo imeendelea kuwatia hofu pindi wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.

Hatua hiyo imekuja ni kutokana na msako ambao unaendelea ziwa Viktoria wa kuwakamata watu ambao wameendelea kujihusisha na shughuli za uvuvi haramu.

Wakizungumza na Mwaandishi wetu baadhi ya wavuvi hao wamesema kuwa pamoja na kuendelea kutii sheria kwa kutumia zana za uvuvi ambazo zinakubalika kwa mujibu wa sheria bado wameendelea kukamatwa na kupigwa faini na watu wa idara ya uvuvi.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho Bi. Anna Peter na Mwenyekiti wa BMU Bw,Peter John wamedai kutokushirikishwa kwenye shughuli hiyo ya kukamata watu hao na kwamba  elimu bado  ni tatizo kwa wavuvi wengi kutokujua ni zana zipi ambazo zinatumika kwenye shughuli zao kutokana na kutokupewa elimu.

Hata hivyo kwa upande wake diwani wa kata hiyo,Masumbuko Nsembe amesema malalamiko ya wavuvi hao amekwisha kuyapeleka halmashauri na kwamba hadi sasa yanafanyiwa kazi.


Mtandao huu  umemtafuta Mkuu wa oparesheni hiyo,Bw Roman Mkenda kwa njia ya simu ambapo amesema   kuwa baadhi ya wavuvi wamekuwa wakikimbia pindi wanapowaona hali ambayo inasababisha  wao kujua kuwa ni  mvuvi haramu na kwamba suala la elimu wamekuwa wakilitoa pindi mtu anapoomba kibali cha kutaka kuwa mvuvi.

DKT. BASHIRU ALLY APITISHWA NA NEC KUWA KATIBU MKUU WA CCM

 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Ikulu jijini Dar es Salaam.

 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akizungumza na wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa NEC wakati akiwasilisha Ripoti ya Uhakiki wa mali za Chama cha Mapinduzi CCM kwa wajumbe hao Ikulu jijini Dar es Salaam


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiimba pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kukabidhiwa makabrasha yenye taarifa za uhakiki wa mali za Chama hicho.

 
 Wajumbe kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC wakishangilia wakati kikao hicho kilipokuwa kikiendelea Ikulu jijini Dar es Salaam.

 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally mara baada ya kumpendekeza  na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.

 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally kwenye meza kuu mara baada ya kumpendekeza  na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.

  
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akiwa meza kuu mara baada ya kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.

  
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally wapili kutoka kulia kwenye meza kuu kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.

 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe wa NEC hawaonekani pichani, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally



Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wajumbe mara baada ya kikao cha NEC Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  

PICHA NA IKULU

Monday 28 May 2018

PICHA: WABUNGE WAKISAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KUFUATIA KIFO CHA MH. BILAGO




Baadhi ya Wabunge wakisaini kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Marehemu Kasuku Bilago.

Awali mapema leo Naibu Spika, Tulia Akson aliahirisha Bunge kutokana na Msiba huo, Mh. Bilago alifariki May 26, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa matibabu.