Mkuu wa mkoa wa Geita,Bi.Fatuma Mwasa.
Serikali
mkoani Geita inaendelea na jitihada za
kukabiliana na upungufu wa madawati na majengo ya kusomea mkoani hapo.
Akizungumza
na storm habari katika hafra iliyoandaliwa
na kamati kuu ya ccm mkoani hapa ya kuzipongeza wilaya zilizofanya vizuri
katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana katika ukumbi wa ‘lenny hotel’ mkuu wa mkoa
wa Geita,Bi.Fatuma Mwassa amesema kuwa amezunguka takribani wilaya zote na kujionea
namna na jinsi ambavyo wanafunzi wamekuwa wakipata shida.
Aidha
katibu wa CCM mkoani hapa, London Muba,ametoa shukurani kwa wilaya zote namna na jinsi ambavyo
ziliweza kushiriki katika zoezi la uchaguzi mkuu na hivyo kutokana na zoezi
kwenda vizuri chama cha mapinduzi kimeamua kutoa hati kwa kila wilaya.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoani hapa Agnas Inyasi amemwomba Raisi John Pombe Magufuli kuona umuhimu wa kuwateulia maeneo
ya uchimbaji vijana ambao wapo mkoani hapa
ili waweze kufanya kazi na kupata fedha za kujikimu.
Kamati ya chama cha mapinduzi CCM mkoani hapa imetoa gari aina ya noah ikiwa ni zawadi kwa wilaya ya mbongwe kutokana na
kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
No comments:
Post a Comment