Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU)
wilayani Bukombe imemtaka mkuu wa wilaya ya
bukombe mkoani Geita, Mh.aman Mwenegoha
kufika mahakamani siku ya
jumatatu machi 14,kwa ajili ya kutoa
ushahidi juu ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi umoja.
Mwenegoha
amepewa wito huo wa mahakama ya wilaya wa kufika ili akatoe ushahidi dhidi ya
mwalimu mkuu wa shule ya msingi umoja
iliyoko kata ya Katente mjini Ushirombo James Nying’ati aliyekamatwa akipokea rushwa kutoka
kwa mzazi Marco Elias ili ampatie nafasi mtoto
wake arudie darasa la saba.
Akizungumza
na storm habari mkuu wa wilaya ya Bukombe, amesema kuwa amepata barua ya
mahakama na yupo tayari kwa ajili ya kwenda kutoa ushahidi juu ya kile ambacho
aliweza kukiona kwa mwalimu huyo.
Kamanda wa takukuru wilaya ya Bukombe, Chuzera Shija
amethibitisha kuwa ni kweli mahakama
imempelekea mkuu wa wilaya hati ya wito(samansi) ili afike mahakama ya wilaya akatoe
ushahidi ikiwa ni kwa mujibu
wa taratibu,sheria na kanuni ili mahakama iweze kupata ushahidi wa kujiridhisha na kisha itoe hukumu ya haki.
Hivi
karibuni mwezi februari TAKUKURU iliweka
mtego na kuweza kumkamata mwalimu huyo mkuu wa shule ya msingi umoja James Nying’ati
aliyeomba rushwa toka kwa mzazi ili ampatie msaada wa mwanaye kurudia darasa la
saba.Shija ameionya jamii iache kabisa
tabia za kutoa, kuomba ama kupokea
rushwa ya aina yoyote.
No comments:
Post a Comment