Thursday 30 June 2016

PICHA: WABUNGE WA UPINZANI WAMALIZA BUNGE LA BAJETI KWA MTINDO MPYA



Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani leo asubuhi wameingia bungeni wakiwa wote wamevalia nguo nyeusi walipohudhuria kikao cha 54 cha Bunge la Bajeti mjini Dodoma.

Baada ya Naibu Spika Dk Tulia Ackson kuingia bungeni na kuongoza dua ya kuliombea Bunge, walianza kunyanyua mabango mbalimbali na kutoka nje.

Wednesday 29 June 2016

RAIS MAGUFULI AFANYA MAREKEBISHO MADOGO KATIKA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA


Uteuzi huo umetenguliwa katika wilaya ya Serengeti ambapo ndg.Emile Ntakamulenga aliteuliwa kimakosa na badala yake amemtea Ndg.Nurdin Babu kujaza nafasi hiyo.

WADAU MBALIMBALI WA ELIMU MKOANI GEITA WAOMBWA KUCHANGIA SUALA LA KUBORESHA ELIMU


Wadau wa elimu Mkoani na wilayani Geita,wameombwa kujitokeza kuchangia suala la elimu, ikiwa ni pamoja na kutoa madawati kwaajili ya kutengeneza mazingira bora ya kupatia elimu kwa wanafunzi.

USHINDI WA MBUNGE WA LONGIDO ONESMO OLE NANGOLE WATENGULIWA

Kesi iliyokuwa inaunguruma kuanzia tarehe 29.02.2016 katika mahakam kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii 

MTOTO AUWAWA KWA KUPIGWA FIMBO NA BABA YAKE WA KAMBO





















                   Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi

Taarifa ya jeshi la polisi imeeleza kuwa mnamo tarehe 27.06.2016 majira ya saa 12:00 jioni katika kitongoji cha Moha kijiji cha Ilungu kata ya Nyigogo tarafa ya Itumbili wilaya ya Magu mkoani Mwanza, mtoto aliyejulikana kwa jina la Julius Leonard miaka [7] mwanafunzi wa chekechea shule ya msingi ilunga aliuawa kwa kupigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na baba yake wa kambo aitwaye Leonard Joseph miaka [32] mkulima na mkazi wa kijiji cha Ilunga.

GESI YA HELIUM YA FUTI ZA UJAZO B ILIONI 54 YAGUNDULIKA TANZANIA

Gesi ya helium ya takribani futi za ujazo bilioni 54 inayoelezwa kuwa adimu duniani, imegundulika nchini Tanzania na kuiweka nchi kuwa miongoni mwa mataifa machache yenye madini mengi na muhimu.

Monday 27 June 2016

CHARLES KITWANGA AKABIDHI RASMI OFISI KWA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akizungumza na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kushoto) pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto meza kuu) akimsikiliza aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga alipokuwa anazungumza na Waziri huyo pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano ofisini humo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa pili kulia) alipokuwa anazungumza kabla ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (wa tatu kulia) kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) mara baada ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (katikati) kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto), aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga wakifurahi jambo mara baada ya Waziri Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano katika tukio lililofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dar es salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (wa pili kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
 

PICHA: BENKI YA CRDB YATOA MCHANGO WA MADAWATI WILAYANI SENGEREMA MKOANI MWANZA



Meneja wa CRDB Benki  Amin Mwakang'ata kushoto akiwa na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema.




Meneja wa CRDB Amin Mwakang'ata akizungmza kwa kina lengo la benki hiyo kutoa maadawati hayo ambapo wametoa madawati 81 yenye thamani ya shilingi milioni tano.



Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosha Crispin Luandaakizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya madawati ambapo ameshukuru kwa masaada huo ambao utasaidia kupunguza changamoto ya madawati.


Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema Chalya Julius amesema katika Halmashauri ya Sengerema ilikuwa na upungufu wa madawati 13499 lakini kwa kushirikiana na wadau hadi kufikia june 24 walikuwa na madawati waliotengeneza ni 5875 ambapo CRDB nao wameonyesha mchango wao.



Katibu Tawala Wilaya ya Sengerema Mariam Seleche akitoa neno la shukrani kwa msaada ambao wameonyesha Benk ya CRDB.

Baadhi ya Madawati yaliyokabidhiwa katika Wilaya ya Sengerema.

Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wilaya ya Sengerema.






Sunday 26 June 2016

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMEFANYA MABADILIKO MADOGO KATIKA SAFU YA WAKUU WA MIKOA NA AMEWATEUA WAKUU WA WILAYA 139.

IMETOLEWA NA KURUGENZI YA MAWASILIANO IKULU LEO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

MAZEMBE WAJA LEO USIKU NA JESHI LA WATU 18



MABINGWA mara tano Afrika, TP Mazembe ya DRC wanatarajiwa kutua usiku wa leo tayari kwa mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji Yanga SC, Jumanne Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

WAZIRI NCHEMBA AWAONYA POLISI MATUMIZI YA NGUVU


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameitaka Polisi kutotumia nguvu kubwa katika mambo yasiyokuwa na manufaa kwa wananchi ila nguvu hizo zitumike kupambana na biashara ya dawa za kulevya kwa maslahi mapana ya taifa.

Friday 24 June 2016

ZOEZI LA UNYUNYUZIAJI DAWA ZA UKOKO MKOANI GEITA LAKUMBWA NA CHANGAMOTO

Wakati zoezi la umwagiliaji wa dawa za kuua mbu maarufu kama dawa za ukoko likiendelea mkoani Geita zoezi hilo limekubwa na changamoto kubwa kutokana na         wananchi kushindwa kutoa ushirikiano kwa wamwagiliaji wakidai kuwa dawa hizo zinasababisha ongezeko la wadudu kama kunguni katika nyumba zao pamoja na kusababisha kupungua kwa nguvu za kiume kwa upande wa wananume.

WAZIRI MKUU WA UINGEREZA ATANGAZA KUJIUZULU


Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu baada ya kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika muungano wa Ulaya. Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atasalia ofisini kwa siku tisini zijayo ndipo angatuke.

WAZIRI MKUUU KASSIM MAJALIWA KUWA MGENI RASMI SHINDANO LA KUHIFADHI QURAN



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhi Quran, Shekh Othman Kaporo (katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu shindano la kimataifa la kuhifadhi Quran litakalohitimishwa Juni 26 mwaka huu Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkuu wa Utendaji wa Jumuiya hiyo Ally Sindo na kulia ni Katibu wa Jumuiya hiyo, Mohamed Ali.



Mtoto mwenye umri wa miaka 8, Khalid Abudhar mshiriki wa shindano la kimataifa la kuhifadhi Quran  kutoka Tajikstan akisoma Quran kwa kichwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya washiriki kutoka nchi mbalimbali watakaoshiriki katika shindano la kimataifa la kuhifadhi Quran litakalofanyika Jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhi Quran, Shekh Othman Kaporo (hayupo pichani). 



Mshiriki wa shindano la kimataifa la kuhifadhi Quran kutoka Bangladesh Ahmed Abdallah akisoma Quran kwa kichwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

Thursday 23 June 2016

BAADHI YA WANANCHI WA KIJIJI CHA BUKUNGU MKOANI GEITA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUCHUKUA SHERIA MKONONI



Kamishna msaidizi wa Jeshi la polisi mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo.



Moja ya nyumba zilizobomolewa na wananchi.

Katika hali isiyo ya kawaida wananchi wenye hasira kali wa kijiji cha Bukungu Kata ya Buzirayombo mkoani Geita wamevamia na kubomoa nyumba kwa madai kuwa watu hao wamekuwa wakifanya uhalifu wa kuvamia wanakijiji katika nyumba zao na kuwaibia mali na fedha hali iliyopelekea kuwahisi kuwa wao ndo wahalifu.

OSCAR JOSHUA AANZA KULIPIGA JARAMBA UTURUKI, CHIRWA NAYE AFANYA MAZOEZI


BEKI wa kushoto wa Yanga, Oscar Joshua Fanuel leo ameanza mazoezi mepesi katika kambi ya timu hiyo mjini Antalya, Uturuki kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe wiki ijayo.

Wednesday 22 June 2016

PICHA MBALIMBALI ZA UFUNGUZI WA UNUNUZI WA PAMBA MSIMU WA MWAKA 2016/17 MKOANI GEITA



Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ukiwasili Wilayani nyangw'hwale tayari kwa mkutano wa ufunguzi wa ununuzi wa pamba msimu wa mwaka 2016/17









Wadau wakifatilia Mutano wa ufunguzi wa ununuzi wa Pamba msimu wa 2016/17



Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa ameketi naMkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga



Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Amani Mwenegoha (kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Nyangh'wale Hussein Kasu.


Baadhi wa wadau mbalimbali wakifatilia Mkutano



Brigedia  jenerali mstaafu Emmanuel Maganga ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma nae alikuwepo katika Mkutano alitoa neno juu ya hali ya kilimo cha Pamba.




Mkuu wa Wilaya ya Nyngh'wale Ibrahimu Marwa akimtambulisha Mbunge wa Jimbo hilo Hussein Kasu.


Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza na Wananchi katika mkutano ya ufunguzi wa ununuzi wa pamba.



Mmoja wa Mkulima wa Pamba akipima pamba yake katika mzani ambao umehakikiwa kuwa na ubora.