Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Geita, Lotson Mponjoli
Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia baada ya kuzama kwenye dimbwi la maji lililopo mtaa wa elimu,kata ya Nyankumbu
mkoani Geita.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa geita Mponjoli
Mwabulambo amesema waliofaliki ni Ladislaus
mwenye umri wa miaka kumi mwanafunzi wa darasa la 4 katika shule ya msingi Mseto pamoja na Adela Jonas mwenye umri wa miaka 3.
Kamanda Mponjoli amesema kuwa baada ya jeshi la
polisi kufika katika eneo la tukio walikuta ndoano na samaki wamevuliwa kwenye
maji kitendo ambacho kinaonyesha kuwa watoto hao walikuwa wanavua samaki.
Hata hivyo storm fm ilimtafuta mwenyekiti wa mtaa huo Hassan Mushora
ambapo baada ya kufanikiwa kufanya nae mazungumzo alisema kuwa taarifa za tukio
hilo kama mwenyekiti alilipata majira ya saa 9 alasiri tayari watoto hao wakiwa
wamepoteza uhai.
Akizungumza na storm habari baba mwenye nyumba Bw.
Paulo Masanja ambapo watoto hao walikuwa wakiishi na mlezi wao wa kike ambaye
hakufahamika jina kwa haraka amesema
siku ya tukio mama huyo aliwatuma watoto wakachote maji kwa ajili ya matumizi
ya nyumbani .
Mmoja wa shuhuda nyumbani hapo Lucia Paulo alisema siku hiyo watoto watatu walienda kufuata maji mmoja
wa watoto hao alirudi na kumwambia mama yake wenzake wamezama ndani ya dibwi ndipo mama huyo aliamua kwenda kuwaangalia na
kuwakuta wamepoteza maisha
No comments:
Post a Comment