Vijana wakiwa kwenye mafunzo ya uchomeleaji.
Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) umekuwa ukichangia kwa
kiasi kikubwa katika utoaji wa fursa za kiuchumi kwa wananchi wanaozunguka
Mgodi huo, ambapo kwa sasa inatekeleza miradi mipya mitatu ambayo ni
uchomeleaji,kilimo na ushonaji.
Kwa leo utaona picha mbalimbali
za mafunzo ya uchomeleaji wanayopewa baadhi ya vijana ambapo watakapofuzu
mafunzo watakuwa na jukumu la kuwafundisha vijana wenzao ikiwa ni njia ya kuweza kuwainua wakazi wa Geita kuona fursa za kiuchumi.
Mafunzo hayo yanatolewa bure na
hapo juu ni picha mbalimbali za vijana wakipata mafunzo ya uchomeleaji.
Huu ni mradi wa kwanza tumeuona kwani pia kuna miradi mingine yenye tija inayofadhiliwa na
Mgodi wa GGM wakishirikiana na Serikali.
No comments:
Post a Comment