Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, wilayani Kilombero
jana lilimkamata mbunge wa jimbo la Kilombero (Chadema), Peter
Lijualikali kwa madai ya kutaka kuingia katika kikao cha Baraza la Madiwani cha
kuapisha na kuchagua mwenyekiti na makamu wake wakati si mpiga kura.
Lijualikali alikamatwa nje ya ukumbi wa halmashauri na polisi na
kuswekwa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya ya Kilombero saa 3.48
asubuhi wakati akiingia kwenye ukumbi huo kama mmoja wa mashuhuda.
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kilombero, Shabaan Mikongolo
alisema mbunge huyo hakutendewa haki na polisi kwa kuwa alifika eneo hilo
kushuhudia matukio ya kuapishwa kwa madiwani.
“Ni kama kuna
maelekezo yalitolewa kwa polisi kuwazuia wabunge, Lijualikali na Devotha Minja
(Viti Maalumu – Chadema) na mwakilishi wa Katibu Mkuu Chadema kutoingia
ukumbini lakini viongozi wengine wa Serikali ngazi ya mkoa na wilaya
waliruhusiwa." Alisema Mikongolo
Pia, polisi walizuia waandishi wa habari na kutaka kuwanyang’anya
kamera zao kwa sababu ambazo hazikuwekwa bayana.
Katika uchaguzi huo, Diwani wa Sanje (CCM), David Ligazo
alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilombero kwa kura 19 dhidi ya
Godfrey Lwena ( CHADEMA) aliyepata kura 18
No comments:
Post a Comment