Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na tuhuma za kujipatia fedha kwa kutumia jina la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Washtakiwa hao
walifikishwa katika mahakama hiyo jana kujibu mashtaka 12 yanayowakabili,
likiwamo la kughushi barua na kuziwasilisha katika vituo vya mafuta wakirubuni
watumiwe kiasi cha fedha ili waweze kupata punguzo la kodi.
Washtakiwa hao ni
mwanafunzi, Issa Mohamed Awadhi (27)
maarufu kama Charles
Robert au Mwamunyange, mkazi wa Ilala, ambaye hakuwapo mahakamani hapo kutokana
na kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kuugua.
Wengine ni Hamisi
Tembo(37) mkazi wa Ilala, mtengeneza mihuri, Nicolaus Obado(32), mkazi wa
Mbagala Kuu na Wakati Mungi (51) mfanyabiashara na mkazi wa Yombo Makangarawe.
Washtakiwa walikana
mashtaka na upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika na kukosa
dhamana. Kesi itaendelea Aprili 11.
No comments:
Post a Comment