Friday 28 July 2017

UZINDUZI WA FILAMU YA MAGWANGALA WAINGIA DOSARI


Meneja Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa Geita,Manase Ndoroma akielezea kutokuwepo kwa ugomvi wa aina yoyote kati ya wasanii na mgodi wa GGM na hatua ambayo wameichukua baada ya kuonekana kuwepo kwa mahudhui ambayo yanaleta uchochezi baina ya wananchi na mgodi.


Mwenyekiti wa chama cha wasanii Mkoani Humo ambaye pia ni moja kati ya wachezaji wa Filamu Hiyo ,Bi,Rosemery Michael(Rose Bonanza )Akielezea namna ambavyo wameweza kuingia hasara kutokana na uwandaaji wa filamu pamoja na uzinduzi.


 Naibu Waziri wa Habari Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura.Akizungumza juu ya kukwama kwa uzinduzi wa Filamu ya Magwangala ambayo imechezewa Mkoani Geita na wasanii pamoja na viongozi wa Serikali. 

GHARAMA YA CHANJO YA HOMA YA INI IMEPUNGUA



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto Ummy Mwalimu

Thursday 27 July 2017

MBUNGE WA GEITA VIJIJINI ATOA NENO JUU YA ENEO LA STENDI YA IHANAMILO



Kahimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita akielezea juu ya utatuzi wa tatizo ambalo limeonekana kwenye kijiji hicho juu ya kuuzwa kwa eneo ambalo lilikuwa limetengwa kwaajili ya matumizi ya stendi.



Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini,Joseph Msukuma akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Ihanamilo Kata ya Nkome wakati za zoezi la kuondoa Vigingi ambavyo viliwekwa kwenye eneo ambalo limetengwa kwaajili ya ujenzi wa Stendi ya mabasi kijijini Hapo.



Wananchi wakifuatilia mkutano.

Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini Mh,Joseph Kasheku Msukuma  ambaye pia ni mwenyekiti wa  chama cha mapinduzi CCM Mkoani Geita ameongoza mamia ya wananchi wa kijiji cha ihanamilo Kata ya Nkome Wilayani Geita kutoa visiki ambavyo viliwekwa na mtu ambaye inasadikika amenunua eneo la kijiji   linalokadiliwa kuwa ni hekari moja na nusu  ambalo lilitengwa kwa matumizi ya stendi kutoka kwa serikali ya kijiji.

Hatua hiyo imekuja  baada ya Serikali ya Kijiji ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho ,Bw Thomas Alila na mtendaji wa kijiji Charles Mbilingi kuuza eneo kwa kiasi cha sh ,Milioni sita (6).
Kwa maelezo ya afisa mtendaji wa Kijiji Charles Mbilingi amesema kuwa tarehe 15 mwezi huu walikaa kwenye kikao na wanakijiji na kuamua kwamba wauze eneo hilo  ili liweze kusaidia ujenzi wa shule.

“Tulikaa kama halmashauri ya Kijiji tukajadili namna ya kutatua changamoto ya kukosekana kwa shule kwenye kijiji chetu tulipojadili tukaonelea kwa sababu tuna eneo ni bora tuliuze ili tuweze kupata pesa ambazo zitasaidia ujenzi wa madarasa na hatukufanya peke yetu 
tuliwashirikisha wananchi wa kjiji wakawa wamekubali”Alisema Mtendaji.

Hata Hivyo kutokana na maelezo hayo ya mtendaji wa Kijiji Mbunge  Msukuma amewaeleza wananchi ambao walikuwa kwenye Mkutano wa hadhara kuwa eneo hilo liliuzwa tarehe tano mwezi huu jambo ambalo yeye alilikataa kutokana na faida ambazo zinaweza kupatikana kutokana na uwepo wa eneo hilo.

“Nimesikitishwa sana na kitendo ambacho kimefanyika cha kuuzwa eneo hilo kiasi cha Shilingi milioni sita (6) na mimi nilimpigia simu mtendaji nikamwambia  azirudishe pesa aende halmashauri kuna maelekezo kwa mkurugenzi na tutambue kuna maeneo muhimu lazima yawepo leo(jana)ninakwenda kung’oa visiki vyote”Alisema Msukuma

Katika hali isiyo ya kawaida  Diwani wa Kata ya Nkome Masumbuko Nsembe amejikuta jina lake likiwa limeandikwa kuwa ni miongoni kati ya viongozi ambao walilidhia  kuuzwa kwa eneo  la kijiji.
“Mheshimiwa Mbunge mimi sikuuza nilifika saa kumi na moja nilikuta wakisoma hiyo taarifa ya kuuza lakini mimi niliwaambia kuwa wasiuze eneo hilo kwa hicho kiasi.”Alisema Diwani

Katika hali isiyo ya kawaida wananchi ambao walihudhuria  kikao hicho cha kukubaliana kuuzwa kwa eneo hilo  walipotajwa majina yao walijikuta wakidai kushindwa kujua hali hiyo imetokana na nini na kama waliingizwa mkenge kwenye mauziano hayo.


Kutokana na hatua ambayo mbunge ameifanya ya kuongeza wananchi kutoa visiki wananchi wameshukuru na kusema kuwa walikuwa hawajui  kama eneo lao limeuzwa.

Tuesday 18 July 2017

TUNDU LISSU ASHAURIWA KUACHA PROPAGANDA NA UPOTOSHAJI



Serikali imemshauri Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kutekeleza wajibu wake kwa kusimamia weledi akiwa kama Wakili wa Mahakama Kuu badala ya kufanya Propaganda kwa kutumia lugha ya kejeli, kuudhi na uchochezi kuituhumnu Serikali kuwa inabana demokrasia nchini.

SERIKALI WILAYANI GEITA KUFIKISHA NISHATI YA UMEME KATA YA KASEME



Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye Kisima cha maji ambacho kimejengwa na mgodi wa Nyamutondo kwenye Kata ya Kaseme Wilayani Geita.


Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi akikagua moja kati ya visima ambavyo aliagiza vijengwe kwenye Kijiji Nyamutondo na mwekezaji ambaye ni mchimbaji mdogo.


Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimuuliza moja kati ya wananchi wa Kijiji hicho Bi, Koku Gerevasi,kama amelizishwa na visima ambavyo vimetengenezwa na Mgodi wa  Nyamutondo.


  Mkurugenzi wa Mgodi wa dhahabu wa Nyamutondo Bw.Martin Benda Kajoro,akikabidhi visima hivyo Kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita na Kuomba radhi kutokana na kushindwa kutekeleza agizo lake la mara ya kwanza. 


Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizungumza na wananchi na kutoa maelekezo ya kutunza visima ambavyo vimejengwa kwa gharama kubwa.


Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akikata utepe ishara ya kuzindua visima hivyo.


Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi,akimtwika ndoo ya maji baada ya kuzindua visima hivyo


Serikali wilaya ya Geita  kufikisha nishati ya Umeme katika Kitongoji cha Nyamutondo kijiji na kata ya  Kaseme kabla ya Mwezi Oktoba mwaka huu ili kuwezesha Pampu za visima vya maji kutumia Umeme na kusambaza maji kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi.

Hatua  hiyo ya Serikali imekuja ni baada ya Kukamilika kwa Ujenzi wa Visima viwili kati ya vinne ambavyo vimechimbwa na wawekezaji wa mgodi wa dhahahu wa Nyamutondo uliopo Kijiji hicho ambavyo vimejengwa kwa gharama ya shilingi Milioni hamsini  na nne (54).

Akizindua visima hivyo na Kukabidhi kwa serikali ya Kijiji  Mwl.Herman Kapufi ,amesema uwezo wa kusukuma maji kwa sasa katika visima hivyo ni mdogo kutokana na pampu ambazo wananchi wanazitumia kwa mikono na kwamba kupatikana kwa nishati ya umeme kutarahisisha na kuboresha huduma ya maji

“Kazi yangu ni kuhakikisha umeme unaletwa hapa ili kurahisisha swala la maji na kufikia mwezi wa Kumi umeme utakuwa umefika kwenye kijiji hiki”Alisema Kapufi.

Naye Mkurugenzi wa Mgodi wa dhahabu wa Nyamutondo Bw.Martin Benda Kajoro amesema kukamilika na kuzinduliwa kwa visima hivyo kutaondoa changamoto ya maji kwa wananchi iliyopelekea kufungwa kwa shughuli za uchimbaji wa dhahabu kushinikiza wawekezaji kuchimba visima.    

“Kweli kulikuwa na shida kubwa sana ya maji lakini kutokana na hali hiyo Mkuu wa wilaya alituagiza kujenga visima virefu vya maji na sisi tulitilia maanani agizo lake na ndio maana leo (jana) tumemaliza na tumekabidhi kwake hivyo tunamwomba tu afikishe kwa afisa madini aweze kutufungulia mgodi wetu maana kwa sasa hatufanyi shughuli zozote”Alisema Kajoro

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho ambao wamezungumza na mtandao wa maduka online ,Semeni John   na Koku Gerevasi wamesema   walikuwa wakikabiliana na changamoto ya kukaa kwenye foleni kwa muda mrefu na wakati mwingine kujikuta wakikabiliana na vurugu.


Friday 14 July 2017

WANANCHI MKOANI GEITA WALILIA MAFUTA







Kufuatia agizo la Waziri wa Fedha na Mipango,Dk Philip Mpango la kuzitaka mamlaka za mapato Nchini (TRA)kufanya ukaguzi nchi nzima ili kubaini  wamiliki wa vituo vya mafuta wanaokiuka maagizo ya serikali yaliyowataka wafunge mashine maalum za kielektroniki za kutolea risiti(EFD)tangu mwaka jana.

Monday 10 July 2017

RAIS MAGUFULI ATOA ONYO KWA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA NA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI AWATAKA WAWE NA NIDHAMU YA PESA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaonya wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya   nchini  kote kuachana na tabia ya kutumia fedha za serikali isivyotakiwa wakati wa  Mkutano ambao umefanyika kwenye  viwanja vya shule ya sekondari  Wilayani Chato 

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamini Mkapa  ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye makabidhiano ya Nyumba za watumishi wa sekta ya afya akizungumza na wananchi ambapo amesisitiza watumishi waliopo kufanya kazi kwa kujituma zaidi.

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamini Mkapa akimkabidhi hati za nyumba hamsini , Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamini Mkapa akimkabidhi,mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Nicas Safari hati ya nyumba za watumishi wa afya.

Mama Janeth Magufuli Akisalimiana na Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Mkutano Wilayani Chato.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mkutano.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Wilaya ya Chato.

Mtendaji Mkuu wa  Mkuu wa taasisi ya Benjamini Mkapa Ellen Senkoro ,akielezea makusudi ya kujenga Nyumba hizo kwenye Mikoa ya Kagera,Simiyu na Geita.

Mbunge wa Chato ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati Mheshimiwa Medadi Kalemani akizungumza na wananchi na kushukuru serikali kwa kuendelea kuwekeza kwenye Sekta ya afya.

Madiwani wa kata mbali mbali Mkoani Geita.

Wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akielezea mikakati ya kuendelea kuboresha sekta ya afya.


Wananchi wa wilaya ya Chato na Wilaya zilizopo Mkoani Geita wakifuatilia Mkutano wa



















Rais Magufuli amesema hayo leo wilayani  Chato mkoani Geita alipokuwa akihutubia wananchi katika makabidhiano ya nyumba 50 zilizojengwa na taasisi ya Benjamin Mkapa, ambapo mbali ya kushukuru kwa msaada huo Rais Magufuli alizungumzia juu ya tabia ya baadhi ya viongozi wa serikali kuiba fedha za wananchi na kutumia katika mambo yao wenyewe nje ya malengo ya serikali.
"Hapa penyewe Chato kuna fedha zaidi ya bilioni moja za pembejeo zimeliwa na viongozi, hivyo natoa wito kwa viongozi wote wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kote nchini kuwa na nidhamu na fedha za serikali, tujifunze kutumia fedha vizuri  za serikali asitokee mchwa huko kula pesa za serikali. Maana hili lililotokea hapa Chato najua limetokea sehemu nyingi na hivyo saizi tunaanza kufanya ukaguzi kila sehemu"alisema Rais Magufuli.
Mbali na hilo Rais Magufuli aliwataka wananchi wa hali ya chini kuwa na amani kwani katika kipindi chote ambacho yeye atakuwa madarakani hataki kuona wala kusikia wananchi wa hali ya chini wakinyanyaswa sababu na yeye ametokea katika maisha hayo hivyo anatambua jinsi wanavyopata shida watu wa kipato cha chini.
"Serikali haiwezi kufanya biashara na masikini, inawaacha matajiri inawasumbua masikini, mimi nimekuwa katika maisha ya shida nimechunga ng'ombe, nimeuza maziwa kwa hiyo najua maisha ni nini. Najua Tanzania watu wengi wanaishi maisha ya chini na katika kipindi changu sitaki kuona watu wa hali ya chini wanapata shida, wanapata taabu ndiyo maana tunajitahidi kuhangaika kuleta maendeleo ili wanufaike na wao" alisisitiza Magufuli
Rais Magufuli akuziacha taasisi ambazo zimekuwa zikitetea wanafunzi kupata mimba na kusema yeye taasisi hizo hazipendi na ameziwekea kizingiti kuwa ikiwezekana zisipewe msaada bali taasisi zinazofanya mambo ya kimaendeleo kama taasisi ya Mkapa Foundation ndiyo zinatakiwa kupewa msaada sana kwa kuwa zinarudi kuleta maendeleo kwa wananchi.
Aidha Kwa Upande Wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema Wizara ya Afya inatarajia kuanza kutoa huduma ya kupandikiza figo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuwapunguzia changamoto wagonjwa kusafiri umbali mrefu nje ya Nchi na matumizi ya pesa nyingi kugharamia matibabu
Aidha kwa Upande wake Rais Mstaafu  wa awamu ya Tatu ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Makabidhiano hayo Benjamini Mkapa,amesema kuwa anatambua kuwa bado nchi inauhaba wa wahudumu wa afya lakini amewataka wale ambao wapo kwa sasa ni vyema kuakikisha wanajituma na kufanya kazi kwa uhadilifu Mkubwa na kwa waledi katika kutoa huduma  kwa wananchi .
Mtendaji Mkuu wa  Mkuu wa taasisi ya Benjamini Mkapa Ellen Senkoro amefafanua kuwa  nyumba hizo ambazo zimejengwa kwenye Mikoa ya Simiyu ,Geita na Kagera ni juhudi ya taasisi hiyo kwa kushirikiana na serikali kupunguza vifo vya wakina mama na watoto hasa ambao wanaishi maeneo ya vijijini.


Wednesday 5 July 2017

WALIMU KUENDELEA KUPATIWA MAFUNZO MAALUM YA KUFUNDISHA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU



Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imesema imeandaa mtaala mpya ambao umeandaliwa katika misingi ya elimu jumuishi ambao ulianza kutumika kuanzia mwaka wa masomo 2014/2015 ili kumudu wanafunzi wenye mahitaji maalum.