Hatimaye uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es Salaam umekamilika leo katika
ukumbi wa Karimjee, na kushuhudia Isaya Mwita wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo.
Mwita ameibuka na
ushindi na kutangazwa kuwa Meya Mpya wa Jiji la Dar es Salaam baada ya kupata
kura 84 akimshinda mpinzani wake, Yenga Omary wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) aliyepata kura 67.
Uchaguzi huo umeweka
historia ambapo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi
(1992), Chama Cha Upinzani kimepata nafasi ya kuongoza jiji hilo.
Uchaguzi huo
uliahirishwa mara kadhaa kutokana na mvutano uliokuwa unaibuka kati ya wajumbe
wa CCM na Chadema na kuzua vurugu wakati mwingine.
Tofauti na ilivyo kwa
tarehe nyingine za uchaguzi zilizopangwa na kuahirishwa wakati wajumbe wakiwa
ukumbini, viongozi wa ngazi za juu wa Chadema pamoja na aliyekuwa mgombea urais
kwa tiketi ya chama hicho, Edward Lowassa walihudhuria kushuhudia uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment