Mratibu
wa TASAF wilayani Mbogwe mkoani Geita Bi.Mercy Joseph Kabaka amewaonya baadhi ya wenyeviti
na watendaji vijiji walioharibu zoezi kwa kuingiza walengwa wa mpango wa
kunusuru kaya maskini wasiokuwa na sifa hizo na kuwataka wahakikishe wanaitisha
mikutano mikuu ya vijiji ili kuwaondoa mara moja.
Bi.Kabaka
amesema kuwa kumejitokeza malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi toka
vijijini wakilalamika kuwa kuna watu wanafaidika na mpango lakini si maskini
kwani walipitisha kimakosa kwa kuangaliwa kuwa ni ndugu, ukoo, chama ama dini
fulani.
Mratibu
huyo amewaonya wanyeviti wa
vijiji kuwa wao ni wanasiasa lakini TASAF si ya kisiasa wala udini
ama ukabila lengo lake kubwa ni kuwasaidia watanzania wanatoka kaya maskini ili waweze kuinuka
kiuchumi lakini imebainika
wao wameipotosha TASAF kwani wameingiza kaya ambazo si maskini hivyo wahakikishe
wanazibaini kaya hizo na kuziondoa haraka.
Kabaka
ameongeza kuwa agizo la waziri Kairuki
wamelipokea na pia amethibitisha kuwa hali hiyo ya kuingizwa kwenye mpango
wasiokuwa na sifa kwa baadhi ya vijiji hali hiyo ipo,kwani tayari katika ofisi
yake wamekwisha pokea malalamiko toka kwa wanajamii kuwa wao ni kaya maskini
lakini majina yao yaliachwa kwa vile wenyeviti na watendaji waliangalia vyama,
ukoo,udini hivyo na wao wanaomba waingizwe kwenye mpango huo.
Wilaya
ya Mbogwe ina jumla ya vijiji 60 ,kaya zipatazo elfu 4,834 na kiasi
cha zaidi ya sh milioni mia moja tisini na tisa, laki tisa arobaini
na saba elfu na sitini na nane (199,947,068.18 ) zinagawiwa katika
vijiji hivyo.
No comments:
Post a Comment