MICHEZO NA BURUDANI

YANGA YAIBUKA KIDEDEA LEO BAADA YA KUIFUNGA SIMBA BAO 2-0

                    Shabiki wa yanga wakishangilia baada ya kuibuka kidedea. 

Kitendawili cha nani mbabe kati ya watani wa Jadi wa Msimbazi na Jangwani kimekamilika baada ya Simba kufungwa bao 2-0 kwa mara ya pili ndani ya miaka miwili, ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Simba ambao walicheza wakiwa pungufu baada ya mchezaji wake Abdi Banda kupigwa kadi nyekunde hatua iliyodhoofisha zaidi nguvu ya wana Msimbazi.

Uzembe wa mabeki wa Simba katika dakika ya 39 ya kipindi cha kwanza ulipelekea kupachikwa goli la kwanza na Donald Ngoma raia wa Zimbabwe. Dakika ya 72 ya mchezo, uzembe wa mabeki wa Simba ulimpa nafasi mshambuliaji Amisi Tambwe kucheka na nyavu zao.

Tambwe ameiadhibu Simba, timu ambayo alimsajili kwa mara ya kwanza alipoingia nchini na baadae kuhamia kwa wana Jangwani. Mchezaji huyo alipachika goli huku walinzi wanne wa Simba wakiwa wanalandalanda katika eneo la goli lao.


Yanga wameweka historia ya kumfunga Simba kwa misimu miwili mfululizo huku ikifuta machungu ya kushindwa kuifunga Simba kwa misimu 10 mfululizo kati ya mwaka 2000 hadi 2009.

No comments:

Post a Comment