Monday 4 June 2018

WANANCHI WA NYAKAGWE WAIOMBA SERIKALI KUWATENGENEZEA DARAJA


Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Nyakagwe wakivuka Mto kwa kuvua viatu kutokana na kukosekana kwa daraja kwenye eneo hilo.


Mwananchi akivusha usafiri kwenye eneo la Mto ambao unapita kijijini Hapo.


Mkuu wa wilaya ya Geita, Mwl Herman Kapufi akiwa na baadhi ya wajumbe wa chama cha mapinduzi (CCM)wakitazama namna ambavyo tatizo hilo lilivyo.

Mkuu wa wilaya ya Geita, Mwl Herman Kapufi akizungumza juu ya mikakati ya kuwasaidia wananchi na tatizo la kukosekana kwa Daraja .
Wananchi wa Kijiji cha Nyakagwe kata ya Butobera Wilayani Geita wameiomba serikali kuwatengenezea daraja la kuvukia kwenye mto unaopita  kijijini hapo kutokana na sasa hivi kujikuta wakipata shida pindi maji yanapojaa kwenye eneo hilo.

Baadhi ya wanakijiji ambao wamezungumza na mtandao huu wameelezea kuwa wamekuwa wakipata shida kubwa pindi mvua zinaponyesha na kusababisha wanafunzi kushindwa kwenda masomoni  pindi mto huo unapojaa maji.

Pindi mvua zinaponyesha mwandishi watoto wetu wanashindwa kwenda masomoni kwani hali inakuwa ni mbaya na maji yana jaa sana kwenye haya maeneo ya juu hivyo tunajikuta tunashindwa namna ya kufanya tunabaki kuwashauri wanafunzi kutokwenda kwenye masomo lakini tunaamini kama serikali itasikia kilio chetu ikatusaidia juu ya hili tutakuwa tumenufaika” Alisema Mzee John Mabisa.

Hata hivyo diwani wa Kata hiyo,Bw  Hemed Swalehe amesema  jitihada ambazo amezifanya kwa sasa ni kuwasiliana na wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) Hili waweze kufika na kujionea tatizo hilo waone namna ambavyo wanaweza kuwasaidia wananchi hao ambao wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu.

Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi amefika kwenye eneo hilo na kujionea tatizo na kuahaidi kuwasiliana na meneja wa TARURA ili aweze kuja na kuona namna ya kutatua tatizo hilo.

“Niseme tu kwamba nitahakikisha Meneja wa TARURA wa Mkoa anakuja na kuona namna ambavyo wanaweza kusaidia ujenzi wa daraja hili ambalo limekuwa ni tatizo la Muda mrefu kwa wananchi wa vijiji hivi viwili kwa maana Butobela na Nyakagwe” Alisema DC Kapufi.

No comments:

Post a Comment