Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano nchini imewapiga marufuku wafanyakazi wake ''Kuchati'' katika
mitandao ya kijamii kwa kutumia simu katika muda wa saa za kazi.
Waziri wa Wizara hiyo Makame Mbarawa amekemea tabia ya baadhi ya
wafanyakazi, kutumia muda mwingi maofisini kuperuzi katika mitandao ya kijamii
pamoja na kupiga porojo, hali inayosababisha kushuka kwa uzalishaji na
maendeleo.
Ameongeza kuwa watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua
za kisheria bila ya kuonewa haya, na pia kuwataka wafanyakazi wa wizara yake kuwa
na bidii ya kazi na weledi.
Lakini hata hivyo, marufuku hiyo itaweza kufanikiwa?, kutokana
na ukubwa wa matumizi ya mtandao, huku walengwa wakiona wananufaika nayo.
Kutokana na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano
duniani, watu wengi hususan vijana wamekuwa wakitumia muda mwingi katika
mitandao ya kijamii, kupitia simu za mikononi na kompyuta, kwa lengo la kupata
taarifa mbalimbali za ulimwengu na pia kujifunza.
Nchini Tanzania matumizi ya huduma ya mawasiliano imekuwa kwa
kasi katika siku za hivi karibuni, hususan kupitia mitandao ya WhatsApp,
Facebook, Twitter na blogi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment