Mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi
kilimani iliyopo mji mdogo wa Katoro wilayani Geita mwenye umri wa miaka 11
amekuwa akifanyiwa kitendo cha ubakaji kwa zaidi ya miezi miwili na mwanaume
mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Joseph.
Amekuwa akirubuniwa na Joseph kwa madai ya kumuahidi
kumuoa na kumhudumia huku akimlaghai kwa kumpa kiasi cha shilingi 1000 hali
iliyosababisha mwanafunzi huyo kuacha kuhudhuria masomo
Mwanafunzi huyo ambaye amekuwa hafiki shule na
alipoulizwa na baba yake mzazi alidai kuwa shule hawafundishwi na ndipo baba
yake aliamua kufatilia kwa karibu na kugundua mtoto wake hahudhurii masomo.
Mmoja wa walimu wa shule ya msingi kalemani ajulikanaye
kwa jina la Jumanne Misungwi alibainisha kupigiwa simu na baba mzazi na
kulalamikiwa kutofundishwa kwa mtoto huyo na ndipo alimuomba mzazi huyo afike
shuleni ili kutatua tatizo hilo sambamba na kupata ukweli.
Katika hatua nyingine mmoja wa walimu wakike ilibidi
amchukue mwanafunzi huyo na kukaa nae chini ili ajue kipi kimemsibu hadi kutohudhuria
masomo.
Aidha jeshi la polisi mkoani Geita limedhibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kwamba linamshikilia mtuhumiwa kwa uchunguzi zaidi na mara
baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani kujibu shitaka hilo.
No comments:
Post a Comment