KUHABARISHA NA KUFAHAMISHA KUHUSU HABARI NA MAMBO YANAYOENDELEA KATIKA JAMII YA GEITA, KANDA YA ZIWA, TAIFA NA DUNIANI. TUTUMIE HABARI AU WASILIANA NASI KUPITIA info@stormfm.co.tz au +255 685 883 870
Wednesday, 17 February 2016
MKAZI MMOJA MKOANI GEITA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUNASWA NA UMEME
Bw.Daudi Boniventure mkazi wa kata ya Nyankumbu mkoani hapa amefariki dunia baada ya kunaswa na umeme alipokuwa akisambaza umeme wa kufua na jenereta.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Geita bw, Ibrahimu Msengi amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa moja na nusu jioni katika mtaa wa Elimu kata ya Nyakumbu.
Ameeleza kuwa marehemu aliyetajwa kwa jina la hilo amekutwa na mauti baada ya waya aliokuwa akitumia kusambaza umeme uligusa katika msongo mkubwa wa umeme wa tanesco hali iliyopelekea kutokea kwa shoti na hatimae kusababisha mauti yake.
Mashuhuda walioshuhudia tukio hilo wamesimulia namna ambavyo lilivyotokea huku wakidai chanzo kinatokana na kukosekana kwa umeme wa tanesco katika baadhi ya maeneo ya mtaani hapo.
Aidha jeshi la polisi mkoani geita limeendelea kutoa wito kwa wananchi wote kuchukua tahadhari ya kutogusa nyaya zilizoinama au kulala chini ili kuepusha vifo vinavyosababishwa na umeme.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment