Tuesday 14 November 2017

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA TAMASHA LA MTANZANIA LILILOANDALIWA NA MGODI WA GGM

DSC_0230

Baadhi ya viongozi wa mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) Wakiwa na nyuso za furahaa wakati wa sherehe za usiku wa Mtanzania.

DSC_0237
Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM) Bw Richard Jordinson (Kulia) akitoa hotuba kwenye tamasha la usiku wa mtanzania  anayetafasiri hotuba hiyo kwa lugha ya Kiswahili ni Meneja wa masuala ya Jamii wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) Bw Manace Ndoroma (kushoto)

DSC_0247


Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM) Bw Richard Jordinson (wa Pili kushoto) akichukua chakula chenye asili ya Mtanzania

DSC_0280

Mkurugenzi Mtendaji waGGM Bw Richard Jordinson(kulia) akitoa tuzo kwa Bi Frola Gobeta(wa Pili kulia) baada ya kutangazwa Mshindi aliyependeza Zaidi katikaVazi la Kitanzania,Akishudia tukio hilo ni Meneja Mwandamizi wa Rasilimali Watu kutoka GGM Bw Charles Masubi

DSC_0282
Mkurugenzi Mtendaji wa GGM Bw Richard Jordinson (kulia) akimkabidhi Zawadi ya Picha, Msanii wa Filamu Bi,Rosemery Michael  baada ya Kutangazwa Mshindi bora kwenye Vazi la Asili.

DSC_0295
Msanii wa Muziki wa Dansi  Christian Bella(Katikati) akitumbuiza kwenyeTamasha la Usiku wa Mtanzania akiwa na Bendi yake.

DSC_0310
Mshereheshaji kwenyeTukio la Usiku wa Mtanzania Stevie Nyerere(kulia) akimtambulisha Msanii Christian Bella(kushoto).

Mgodi waDhahabuGeita (GGM) umeadhimishaTamasha la Usiku  wa Mtanzania Jumamosi Tarehe 11 Novemba kwenye Ukumbiwa Desire Park Mjini Geita.

Akizungumza wakat iwaTamasha hilo linaloutambulisha utamaduni wa Mtanzania,Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodiwa Dhahabuwa Geita Bw Richard Jordinson amesema kuwa Tamasha hilo limeandaliwa kwa ushirikiano waGGM,JamiiyaWatuwa Geita, Wakandarasiwa Ndani,Watoa huduma na wadau mbalimbali wanaofanya kazi na Kampuni ya GGM mjini Geita.

“Tamasha la UsikuwaMtanzanialilianzishwarasmimwezi April mwaka 2002 likisherehekewa pamoja na Sikukuu ya Muungano likikutanisha wafanyakazi Watanzania wanaofanyakazi ndani ya Mgodi wa Dhahabu Geita,BaadayeTamasha hilo lilifanyiwa marekebisho na kuanza kuadhimishwa mwezi Oktoba hadi Novemba kila mwaka ili kumuenzi pia Baba waTaifa la Tanzania Hayati Julius Kambarage Nyerere aliyefariki Dunia Oktoba 14 mwaka 1999”alisema Bw Jordinson 

Bw Jordinson alisema kuwa GGM inajivunia kufanya kazi ndani ya Tanzania,nchi iliyoasisiwa kwenye misingi mikubwa ya Amani,umoja naUshirikiano,hivyo tukio hilo nikumbukumbu muhimu ya kuenzi utamaduni wa Mtanzania.

.
Akitangaza Washindi Mbalimbali walio valia vizuri mavazi yenye asili ya Kitanzania kwenyeTamasha hilo,Meneja Rasilimali Watu wa Mgodi wa Dhahabu Geita Bw Charles Masubi alisema kuwa Tamasha hilo ni fursa pia ya kutambua utamaduni wa Mataifa mbalimbali yanayo fanya kazi ndani ya Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM)

“GGM ilianza rasmi shughuli zake mwaka 2000 ikiwa na mchanganyiko wa Wafanyakazi kutoka mataifa mbalimbali,Mkurugenzi Mkuu wetu kipindi hicho Hayati Harry Michael alianzisha utaratibu mzuri wa kila taifa kuwa na siku yake ya kuenzi utamaduni wao.

Tamasha la Usiku wa Mtanzania linatukutanisha pia na Jamii ya Watu wa Geita na Mataifa mengine kujifunza utamaduni mzuri wa Taifa la Tanzania vikiwemo vyakula vya asili,ngoma,burudani na maonyesho”alisemaBwMasubi.

Akitoa neno la Shukrani,Meneja mwandamizi wa GGM anayeshughulikia masuala ya Jamii Bw Manace Ndoroma alisema kuwa Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM) unatambua umuhimu mkubwa wa Jamii ya Watuw a Geita ndiyo maana umelifanyaTamasha hilo katikati ya Jamii ya Geita ilikutoa fursa pia ya wao kujivunia Utamaduni wa Mtanzania

“Hizi ni jitihada kubwa za kukuza ujirani mwema kati yetu na Jamii ya Watuwa Geita.GGM inafarijika sana kuandaaTamasha kubwa la Usiku wa Mtanzania na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya Watanzania waishio mkoani Geita”alisemaBw Ndoroma

No comments:

Post a Comment