Chuo
cha ukunga na uuguzi cha Grobal Community kilichopo Wilaya na Mkoani Geita kinalalamikiwa na wanafunzi wake
kutokuwa na usajili.
Wakizungumza
na storm habari kwa nyakati tofauti chuoni hapo,wamesema kuwa wamekuwa na wasi
wasi na chuo hicho ni kutokana na mtaala wa masomo kutofautiana na vyuo vingine
vya uuguzi pamoja na kutokupata ushirikiano pindi wanapokuwa katika masomo ya
vitendo hususani katika hosptali na zahanati za serikali kwani wamekuwa
wakiambiwa hawatambuliki.
Mmoja
kati ya wanafunzi waliohitimu katika
chuo hicho mwaka jana Rosemerry Jacktone,amesema kuwa anasikitishwa kwa kutokupatiwa cheti cha kumaliza tangu
mwaka jana hali ambayo imeendelea kuwapa
wasi wasi na kuwanyima fursa za kuangalia ajira kutokana na kutokuwa na cheti
cha chuo.
Aidha
Mkurugenzi wa chuo hicho, Bw.Denis Joel
akizungumza na storm habari amesema kuwa chuo chake kimesajili wasiwasi wake anajua kuwa wale wanao kizonga
chuo hicho ni baadhi ya watu wenye chuki
na maendeleo.
Kwa
upande wake kaimu mganga mkuu ,Mabera Ezekiel ameeleza kuwa kwa uhalisia uliopo katika chuo hicho ni
kweli hakijasajiliwa kwani malalamiko ya wanafunzi yameshafika katika ofisi ya
mganga mkuu muda mrefu na walikiomba chuo hicho kuhakikisha kuwa
kinapeleka nyaraka ambayo inatambulika
kuwa chuo hicho kimesajiliwa.
No comments:
Post a Comment