Wednesday 31 August 2016

RAIS MAGUFULI AMTHIBITISHA BW.GERSON MSIGWA KUWA MKURUGENZI WA MAWASILIANO IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemthibitisha Bw. Gerson Partinus Msigwa kuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, (Director of Presidential Communication - DPC).

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Agosti 31,2016 na Katibu Mkuu Ikulu Bw. Peter Ilomo imeeleza kuwa Bw. Gerson Partinus Msigwa amethibitishwa kuanzia leo tarehe 31 Agosti, 2016 kushika wadhifa huo.

Kabla ya uthibitisho huo, Bw. Gerson Partinus Msigwa alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, katika Ofisi ya Rais Ikulu kuanzia tarehe 17 Novemba, 2015.

Jaffar Haniu
Kaimu Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi.
Dar es Salaam
31 Agosti, 2016


PICHA:WAZIRI NAPE AKUTANA NA UMOJA WA VYAMA VYA WAALIMU WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA(SATO)



 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimia na Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mkoba walipokutana katika ufunguzi wa mashindano ya michezo ya Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini mwa Afrika (SATO)yaliyofanyika Agosti 30,2016.



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akimsikilza Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mkoba walipokuwa wakijadiliana maswala mbalimbali ya kimichezo katika ufunguzi wa mashindano ya michezo ya Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini mwa Afrika(SATO) uliofanyika Agosti 30,2016. 



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kushoto) akizungumza na viongozi wa Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) katika ufunguzi ya mashindano ya michezo ya Umoja huo uliofanyika Agosti 30,2016.



Katibu Mkuu wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Bw. Yahya Msugwa(kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kushoto) walipokutana katika ufunguzi wa mashindano ya michezo ya Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) uliofanyika Agosti 30,2016.



Rais wa Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini mwa Afrika(SATO) Bw. Henry Kapenda akielezea jambo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa pili kushoto) walipokutana katika ufunguzi wa mashindano ya michezo ya Umoja wa Vyama vya Waalimu wa nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) uliofanyika Agosti 30,2016. 

SERIKALI YASHIKILIA MSIMAMO KUPINGA NDOA ZA JINSIA MOJA.



Naibu Mwanasheria mkuu wa Serikali Mhe. Gerson Mdemu akiongea na wajumbe kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia wakati wa ufungaji wa kikao kuhusu mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa, Leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Masuala ya Katiba na Haki za Binadamu Kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Sarah Mwaipopo.




Wajumbe kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia wakimsikiliza Naibu Mwanasheria mkuu wa Serikali Mhe. Gerson Mdemu wakati wa ufungaji wa kikao kikao kuhusu mapendekezo yaliyotolewa kwa serikali wakati wa majadiliano ya taarifa ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu chini ya mfumo wa mapitio kwa kipindi maalum na baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa, Leo Jijini Dar es Salaam.

MBOWE ATANGAZA KUAHIRISHA MAANDAMANO YA OPARESHENI UKUTA YALIYOKUWA YAMEPANGWA KUFANYIKA KESHO



Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ametangaza kusitishwa kwa maandamano ya Oparesheni UKUTA yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kesho nchi nzima.

Monday 29 August 2016

SERIKALI YAFUNGIA VITUO VIWILI VYA REDIO NCHINI







Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akitoa tamko la kufungia vituo viwili vya redio ambavyo ni Kituo cha Redio Five Arusha  na Magic  FM Dar es Salaam kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kutokana na  kukiuka Kanuni za Sheria ya Utangazaji ya mwaka 2005 kwa kurusha hewani vipindi vyenye maudhui ya uchozezi,na Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Vyombo vya Habari Bw. Jamal  Zuberi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.



Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia tamko alilokuwa akitoa Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) la kufungiwa kwa Redio  Five  Arusha na Redio Magic FM Dar es Salaam leo Agosti 29,2016 Jijini Dar es Salaam.

WADAU WA MICHEZO NCHINI WASHAURIWA KUWEKEZA KATIKA VIWANDA



Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na wadau wa Michezoalipokuwa akizindua  uzinduzi wa Channeli mpya za Michezo kutoka kampuni ya TING Agosti 28,2016.



Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya TING Dkt .Veron Fernandez akielezea kuhusu faida za channeli mbili mpya  za michezo kutoka katika kampuni yake zitakavyosaidia kukuza Michezo nchini Agosti 28,2016.



Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya TING Dkt. Veron Fernandez wakati wa uzinduzi wa Channeli mbili za Michezo kutoka Kampuni ya TING Agosti 28,2016.



Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikata utepe kuashiria  uzindua  wa Channeli mbili za michezo ambazo ni  TING Michezo HD 1 na TING Michezo HD 2 kutoka Kampuni ya TING Agosti 28,2016.




Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw.Said Kiganja akionesha zawadi ya King’amuzi aliyopewa na Kampuni ya TING wakati wa uzinduzi wa Channeli mbili za Michezo kutoka Kampuni hiyo Agosti 28,2016.

Sunday 28 August 2016

MAGUFULI:NI MUUJIZA KUSHIKANA MKONO NA LOWASSA


Rais Magufuli amesema anashukuru hafla ya Jubilei ya Miaka 50 ya ndoa ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa kuleta muujiza wa kukutana na kupeana mkono na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa

Kauli hiyo aliitoa jana katika hotuba yake Baada ya kumalizika kwa misa takatifu ya maadhimisho ya Juibilei hiyo iliyofanyika katika kanisa la mtakatifu Petro  Oysterbay, Dar es Salaam

Friday 26 August 2016

MIGOGORO YA FAMILIA YASABABISHA KIFO CHA MTU MMOJA MKOANI GEITA



Mtu  mmoja amejinyonga kwa kamba ya manila na kupoteza maisha kwa kile kinachosadikika kuwa ni migogoro  wa  kifamilia kati ya mke na mume.

MAFUNDI WA TEMESA KUTUMIA MAFUNZO WALIYOPATA KUENDANA NA KASI YA TEKNOLOJIA



Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri(katikati aliyesimama) akizungumza na mafundi wa TEMESA wakati akifunga mafunzo ya mafundi wa Wakala hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.



Kaimu Mtendaji TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan(kulia) akitoa neno kwa mafundi wa TEMESA wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016 kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri .


Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akionesha moja ya vifaa vilivyokabidhiwa na mafundi wa TEMESA kwa ajili ya karakana zao wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.





Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akikabidhi cheti kwa mmoja wa mafundi Bw.Saidi Waziri kutoka Arusha wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.



Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akikabidhi moja ya vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya karakana za TEMESA kwa Bw. Japhet Mwita mmoja wa washiriki wa mafunzo yaliyofanyika hivi karibuni katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.





Baadhi wa mafundi wa Temesa kutoka mikoa mbalimbali nchini wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.

Mafundi wa TEMESA wameshauriwa kutumia mafunzo waliyoyapata kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika utengenezaji magari na vifaa vya umeme.

Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Bodi ya Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi Wakala hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri amesema kuwa Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA imedhamiria na kuhakikisha kuwa magari na mitambo yote ya Serikali inatengenezwa kitaalam ili kuleta tija na thamani halisi ya fedha iliyokusudiwa pamoja na kukidhi kiu na matarajio ya wateja.

”Napenda kuwakumbusha kwamba mnayo dhamana kubwa ya kutengeneza magari ya Serikali hivyo kwa mafunzo mliyoyapata ninaamini mmejenga uwezo wa kutosha wa kuhudumia magari na vifaa vya umeme kwa kutumia mfumo wa kisasa” alisema Mhandisi Mashauri.

Ameongeza kuwa ni fursa pekee kwa mafundi waliopata mafunzo hayo kwenda kuwafundisha wenzao ambao hawakuweza kupata mafunzo hayo ili kuongeza kasi ya kutengenza magari na vifaa vya umeme na kupunguza changamoto zilizopo katika utengenezaji magari kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Aidha Kaimu Mtendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan amewashukuru washirika wa TEMESA wakiwemo Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kampuni ya Superdoll kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo ambayo yataleta chachu ya utendaji kazi wa mafundi na karakana za TEMESA zilizopo nchini nzima.

Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kampuni ya Superdoll waliandaa mafunzo ya siku 14  yaliyoanza Agosti 9 na kumalizika Agosti 26, 2016 yaliyoshirikisha jumla ya mafundi 25 kutoka mikoa mbalimbali ili kuwapa uwezo wa kutengeneza magari kwa kutumia mifumo ya kisasa.







WATU 3 WAKUTWA WAMEFARIKI HUKU BAADHI YA SEHEMU ZA MIILI YAO KULIWA NA WANYAMA MKOANI GEITA

Watu 3 wamegunduliwa wakiwa wamefariki  huku  baadhi ya sehemu za miili yao kuliwa na wanyama katika eneo la mlima Kitongo  wilaya ya Nyangwhale mkoani Geita.

MAJAMBAZI YAUA 1 MKOANI GEITA


Mtu  mmoja ameuawa kwa kupigwa na watu wasiojulikana katika eneo la mtaa wa Miti mirefu wilaya na mkoa wa Geita.

SAMATTA APIGA BAO SAFI NA KUTINGA HATUA YA MAKUNDI EUROPA LEAGUE 2016


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amefunga bao la kwanza timu yake, KRC Genk ya Ubelgiji ikishinda 2-0 na kufuzu hatua ya makundi ya Europa League usiku huu.

Thursday 25 August 2016

WAZIRI JENISTA MHAGAMA KUFUNGUA MAONYESHO YA WAJASIRIAMALI



Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Benga’i Issa wa kwanza kulia akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu maonesho ya wajasiriamali yataofanyika Septemba 26 mwaka huu jijini Dar es salaam , kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta  Binafsi nchini (TPSF) Bw. Godfrey Simbeye.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta  Binafsi nchini (TPSF) Bw. Godfrey Simbeye kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu maonesho ya wajasiriamali yataofanyika Septemba 26 mwaka huu jijini Dar es salaam, kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Benga’i Issa.

SAMATTA AWANIA TIKETI YA MAKUNDI EUROPA LEAGUE LEO


MSHAMBULIAJI wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta leo anatarajaiwa kuiongoza timu yake katika mchezo wa marudiano hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Europa League dhidi ya Lokomotiva Zagreb ya Croatia Uwanja wa Luminus Arena, Genk.

MKWASA 'AMFUNGIA VIOO' THOM ULIMWENGU ULIMWENGU TAIFA STARS



KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa hajamuita mshmabuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Thomas Emmanuel Ulimwengu katika kikosi cha wachezaji 20 watakaosafiri mwishoni mwa mwezi huu kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.

UTEUZI MWINGINE WA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI HII LEO AUGUST 25 2016

Leo August 25 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amemteua Andrew Wilson Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Kabla ya uteuzi huo Bw. Andrew Wilson Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu Tanzania (BOT).
Andrew Wilson Massawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Modestus Francis Kipilimba ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Uteuzi wa Bw. Andrew Wilson Massawe unaanza mara moja.

Wednesday 24 August 2016

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI KATIKA IDARA YA USALAMA WA TAIFA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Agosti, 2016 amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Modestus Francis Kipilimba alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Dkt. Modestus Francis Kipilimba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Rashid Othman ambaye amestaafu.

Dkt. Modestus Francis Kipilimba ataapishwa leo mchana tarehe 24 Agosti, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Bw. Robert Msalika kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Robert Msalika alikuwa Afisa Ubalozi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bw. George Madafa kuwa Balozi na nchi atakayopangiwa itatajwa baadaye.

Wakurugenzi na Naibu Wakurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa waliopo wanaendelea na nafasi zao.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam

24 Agosti, 2016

Sunday 21 August 2016

SERENGETI BOYS YAIPIGA AFRIKA KUSINI 2-0 NA KUSONGA MBELE MICHUANO YA AFRIKA

TIMU ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania imefuzu hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Afrika mwakani Madagascar, baada ya kuifunga Afrika Kusini mabao 2-0 jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Friday 19 August 2016

RAIS JOHN MAGUFULI AMUAPISHA MRISHO GAMBO KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA HII LEO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya tukio la Kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wa kwanza (kulia) na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa  na Serikali za Mitaa TAMISEMI Selemani Jafo wa kwanza (kushoto).


 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Donald Kaberuka aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Donald Kaberuka mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 

WAENDESHA PIKIPIKI(BODABODA) WILAYANI MBOGWE MKOANI HAPA WALALAMIKIA JESHI LA POLISI


Waendesha  Pipikipi maarufu kwa jina la bodaboda wa Masumbwe Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita wamelalamikia jeshi la Polisi  wilayani humo kutokana na baadhi ya askari  wa jeshi hilo kukamata pikipiki zao mara kwa mara na kuwaacha na hali ya umasikini inayosababisha kukoswa fedha za kuhudumia familia zao

WATU WAWILI MKOANI GEITA WAUWAWA KWA KUCHOMWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA



Watu  wawili wameuawa kwa kuchomwa moto na watu wasiojulikana kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wavuvi haramu waliokuwa wakifanya shughuli za uvuvi kwa kutumia sumu katika ziwa Victoria na kisha watu hao kubomoa  nyumba za mrehemu hao hali ambayo imewalazimu askari kutumia silaha kali ili kuwatawanya watu hao.

PICHA:RAIS MAGUFULI AMPA BASKELI YA MATAILI MATATU MLEMAVU