Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limemfukuza kazi askari wake kwa
kudaiwa kumtorosha mtuhumiwa wa mauaji katika kituo cha Luguru wilayani
Itilima, mkoani humo huku pia, likiwashikila askari saba wanaodaiwa kuwatorosha
watuhumiwa wengine watatu wa mauaji na ujangili wilayani Meatu kwa uchunguzi
zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda
wa Polisi mkoani Simiyu, Onesmo Lyanga alisema askari huyo amefukuzwa kazi kwa
kulifedhehesha jeshi na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
“Februali 2, mwaka huu
katika Kituo cha Polisi Lugulu, askari alimtorosha mtuhumiwa wa kesi ya mauaji
Itl/Ir/95/2016, mkazi wa Kijiji cha Gambasingu wilayani Itilima,” aliema Kamanda Lyanga.
Aliongeza kuwa polisi wanaendelea kuchunguza tukio la kutoroka
kwa watuhumiwa wa ujangili wilayani Meatu, na linaendelea kuwashikilia askari
wengine saba.
Alisema tukio hilo lilitokea Januari 19, 2016, usiku katika
Kituo cha Polisi Wilaya ya Meatu mkoani hapa na kusababisha watuhumiwa hao
kutoboa ukuta na kutoka.
Kamanda huyo aliwataja watuhumiwa waliotoroka kuwa ni mkazi wa
kijiji cha Mwasungula aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji na wengine wawili
ni wakazi wa kijiji cha Sapa wanaotuhumiwa kukutwa na pembe za tembo.
“Watuhumiwa
waliotoroka katika mahabusu siyo ambao walihusika kutungua helkopita na
kusababisha mauaji ya rubani Rogers Gower, raia wa Uingereza kama baadhi ya
vyombo vya habari vilivyo ripoti, watuhumiwa hao wapo,”alisema Lyanga.
No comments:
Post a Comment