Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr, John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wilayani Chato mkoani Geita |
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr,John
Pombe Magufuli amezitaka kamati zote za shule kuhakikisha kuwa zinasimamia
swala la nidhamu na utoro katika shule
wanazoziongoza na kama kuna
kamati yoyote ambayo itashindwa ni vyema ikajihuzuru mapema.
Wito huo ameutoa
mapema leo wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Chato mkoani Geita,katika
shule ya sekondari Chato,ambapo amesema
kuwa kwa kamati yoyote ambayo itashindwa
kuhakikisha kuwa inadhibiti suala la nidhamu mashuleni ni vyema ikajiondoa
mapema.
Rais Magufuli
amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na wazazi kuhakikisha kuwa wanawafatilia watoto pindi wawapo shuleni ili kuweza kutengeneza Tanzania ya wasomi zaidi.
Aidha wananchi wilayani humo,wamemshukuru Rais Magufuli kwa
ujio wake huku pia wakimpongeza kwa
uchapakazi wake uliotukuka na kwamba wamemwomba kuendelea kuwaondoa watumishi
wote ambao hawana maadili ya kazi.
Rais,Magufuli
amewataka watanzania kuendelea kupendana
na kuwa wamoja na kuachana na fujo
na malumbano ambayo yanaweza kupelekea kutowesha amani ya nchi.
No comments:
Post a Comment