Shirika la umeme Tanzania(TANESCO)
Wananchi wilaya na mkoa wa Geita wamelishukuru shirika la
umeme nchini (TANESCO) kwa kuwasilisha maombi ya kushusha bei ya umeme kwa
asilimia 1.1 katika mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji (EWURA) pamoja na
kuondoa kabisa gharama za maombi ya awali ya wateja wapya na gharama za huduma kwa wateja
wa majumbani.
Storm habari imezungumza na wananchi hao ambao
wamedai kuwa kufanya hivyo kutawasaidia kupunguza bajeti ya matumizi ya umeme
hasa kwa wajasiriamali wadogo na wananchi wenye kipato cha chini kutokana na
kulipa kiasi kikubwa cha malipo na umeme huo kutofika mwishoni mwa
mwezi mwingine.
Naye meneja wa Tanesco mkoa wa GeitaBbw.Joachim Ruweta
amesema kuwa amelifurahia tamko hilo ambalo litakuwa lina unafuu kwa wateja
wake na kwamba wamelipokea uzito mkubwa na tayari limeshapelekwa kwenye taasisi
husika kwa ajili ya kupunguza gharama hizo.
No comments:
Post a Comment