Mkuu wa mkoa wa geita meja Jenerali mstaafu Ezekile Kyunga, ametoa
wito kwa taasisi,mashirika na watu binafisi kujitokeza katika kuunga mkono swala la elimu mkoani
hapa.
Wito huo
ameutoa wakati wa makabidhiano ya mabati 300 kwa ajili ya kuezekea
madarasa katika wilaya ya Geita
yaliyotolewa na mfuko wa hifadhi
wa LAPF ambayo yamegharimu kiasi cha Sh.milioni saba.
Amesema kuwa
ni vyema kwa taasisi ,na mashirika ya watu kujitolea kwa moyo binafsi na
wa dhati kuchangia swala la elimu ili kuweza
kuwawezesha vijana kuwa katika mazingira mazuri ya kusomea.
Aidha kwa upande wake meneja masoko na mawasiliano wa mfuko huo wa
penisheni, James Mlowe,ameeleza kuwa sababu za kutoa msaada huo wa mabati ni
kutokana na changamoto za upungufu wa madarasa ,hivyo wao wameona ni vyema kutoa mabati hayo.
Afisa elimu wa wilaya Deus Seif,amegusia swala la uhaba wa vyumba
vya madarasa ambapo amesema kuwa kwa sasa jumla ya madarasa yaliyopo ni 1585 na
vyumba vinavyoitajika ni 3715.
No comments:
Post a Comment