Wakulima
zao la pamba wapatao 70 waliolima na kupanda pamba eneo linalokadiliwa ekari
250 wilayani Mbogwe mkoani Geita wamepata changamoto ya kupata viuatilifu vya
zao hilo kutokana na taarifa zao kutokuwepo ofisi za vijiji vyao na
idara ya kilimo.
Hali
hiyo imejitokeza kutokana na wakulima hao kupata mbegu za pamba kutoka vyanzo
vingine tofauti na huduma ya ugawaji ya pembejeo za pamba iliyokuwa
inatolewa na umoja wa makampuni ya kuchambua pamba umwapa.
Wakulima
hao wameiomba serikali kupitia idara ya kilimo na bodi ya pamba
iwasaidie ili kuwashawishi UMWAPA
wawaingize kwenye orodha ya daftari la kilimo cha mkataba ili wapatiwe huduma
hiyo muhimu.
Steven
Shilemba kaimu afisa kilimo wilayani Mbogwe amethibitisha kuwepo kwa wakulima
hao 70 ambao wamepata changamoto ya
kutopata viuatirifu kwa wakati.
Wakulima
hao wamepata mbegu za pamba kwa kununua sehemu zingine na wengine kutumia mbegu
iliyokuwa imebaki msimu uliopita kutokana na tatizo la mbegu
zilizoanza kusambazwa na UMWAPA kuwa
na uotaji hafifu.
Aidha
shilemba amewataka wakulima hao wavute subira kwani serikali kupitia
idara yake ya kilimo na bodi ya pamba wanaendelea kupata idadi halisi ya
wakulima wenye uhitaji huo ili UMWAPA
wawape viuatilifu hivyo.
Afisa
huyo amethibitisha tayari wakulima waliokosa wameanza kupelekewa viuatilifu ili
kudhibiti wadudu wa zao la pamba.
Shilemba
amesema, kuwa kwa msimu huu wa kilimo wilaya ya mbogwe ina wakulima waliolima
pamba wapatao elfu nane miatano na 3
ambao wamelima jumla ya hekta zinazokadiriwa kufikia elfu 12, au ekari elfu 30,
sawa asilimia 64 ya utekelezaji wa kulima hekta elfu 18, 819.
Makampuni
yanayounda UMWAPA ni 1.Kahama oil
mills ltd (kom) ,2.Nida textile co ltd ,3.Fresho investment co ltd ,4.Kahama
cotton company ltd (kccl) ,5.S.m holdings na 6.Birchand co ltd.
No comments:
Post a Comment