Tuesday 29 August 2017

SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUFANIKISHA TANZANIA YA VIWANDA





Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema serikali inathamini mchango wa sekta binafsi na itaendelea kushirikiana nayo katika kuhakikisha azma ya Tanzania ya viwanda inafikiwa.
Dkt. Mpango alisema hayo Jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akizindua kitabu cha Safari ya Tanzania kuelekea katika Uchumi wa Viwanda 2016- 2056, kilichoandikwa na watanzania wazalendo Bw. Ali Mufuruki, Gilman Kasiga na Moremi Marwa.

‘’Kitabu hiki ni kama mkombozi kwa sisi watunga sera kwani kitatusaidia katika kuyafanyia kazi mapendekezo ambayo yametolewa ili kuhakikisha Tanzania ya viwanda inawezekana, nimewaelekeza pia Tume ya Mipango na Idara ya sera katika Wizara ya Fedha kuchukua mapendekezo ambayo wataona yataisaidia serikali katika kutekeleza azma yake ya kuendeleza viwanda’’alisema Dkt. Mpango

Bw. Ali Mufuruki mmoja wa watunzi wa kitabu hicho alisema wameamua kuunganisha mawazo yao pamoja na kutumia utaalamu na uzoefu wao katika masuala mbalimbali ya maendeleo na uchumi ili kuisaidia serikali kuweza kuondokana na uchumi unaotegemea kilimo na hatimaye kuwa nchi ya viwanda.

‘’Kuna changamoto nyingi zinazozikabili nchi zinazoendelea ikiwemo ukosefu wa utaalamu katika kilimo cha kisasa, ukosefu wa mitaji pamoja na kutokuwa na teknolojia ya kutosha hivyo kwa kuwa azma ya Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni kuwa na nchi ya uchumi wa kati unaotegemea viwanda, tukaona tumuunge mkono katika kutimiza ndoto hiyo kwa kuandika kitabu hiki’’ alisema Mufuruki.

Bw. Mufuruki alisema kuna mambo mengi mazuri ya kulisaidia taifa ambayo yameainishwa katika kitabu hicho hivyo ni vyema watanzania wa kawaida, wasomi, wachumi na hata wawekezaji wakakisoma ili kuona kila mmoja katika nafasi yake anawezaje kuisaidia nchi kutoka hapa ilipo na kufikia katika malengo iliyojiwekea.

Kwa upande wake Bw.Gilman Kasiga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya General Electric katika ukanda wa Afrika Mashariki, alisema ni vyema Tanzania ikawekeza katika masomo kwa kutambua vipaumbele kama inavyofanya nchi ya Ujerumani ambapo sio kila anayesoma ni lazima afikie ngazi ya shahada ndipo aonekane anaweza kuleta mchango katika maendeleo.

Bw. Kasiga alisema asilimia 70 ya wanaomaliza shule hapa nchini wanakimbilia kusoma shahada na kusahau kwamba kuna masomo mengine katika ngazi za astashahada na cheti ambayo kama yakifundishwa kwa umakini na kwa kuzingatia fani husika yanaweza kuzalisha wataalamu wengi ambao wataisaidia nchi kupiga hatua kimaendeleo na pia wao kupata ajira kwa urahisi katika viwanda.


Alisema elimu ya vyuo vikuu ni ya kuandaa wasimamizi yaani mameneja na sio watendaji au wafanya kazi na mafundi hivyo ameshauri mitaala ya vyuo iendane na ukuaji wa viwanda ili wataaalamu hao waweze kutumia taaluma zao katika kulitumikia taifa.



PICHA: NAIBU WAZIRI ANGELINA MABULA AFANYA ZIARA WILAYA ZA BUKOMBE, MBONGWE NA NYANG'HWALE



Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula akiwasili kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Geita na akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa huo  Nyuma yake ni mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa ,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga 


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula,akisaini kwenye kitabu cha wageni ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Mbongwe.


Mkuu wa Wilaya ya Mbongwe Mathar Mkupasi akisoma taarifa ya ardhi na maendeleo ya ukusanyaji wa mapato ambayo yanatokana na ardhi pamoja  majengo yaliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya Hiyo.


Watumishi wa halmashauri ya Mbongwe pamoja na kamati ya Ulinzi na usalama wakifuatilia kikao cha Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbongwe  Elias Kayandabila akionesha mchoro na  ramani ya nyumba ambazo zinatarajia kujengwa na shirika la Nyumba la Taifa.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbongwe  Elias Kayandabila akikabidhi ramani kwa meneja wa shirika la Nyumba Mwanza,Simiyu na Geita Mhandisi Benedict Kilimba .


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula,akikagua mafaili kwenye ofisi za Ardhi za Wilaya hiyo.


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula,akiangalia ramani ya Kijiji cha Bukandwe ambacho kipo kwenye Wilaya ya Mbongwe Mkoani Geita.


Mkuu wa Wilaya ya Mbongwe  Mathar Mkupasi akiagana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula wakati alipotembelea kijiji cha Bukandwe.


Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Josephat Maganga akisoma taarifa fupi ya Wilaya ya Bukombe kwa Naibu  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.


Naibu  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akikagua na kupatiwa maelezo na afisa ardhi mteule Joseph Kimondo .


Naibu  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula ,akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Bukombe.


Monday 28 August 2017

MAAGIZO YA RAIS JOHN MAGUFULI KWA TAKUKURU


Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Makao Makuu ya TAKUKURU jijini Dsm alipofanya ziara leo Agosti 28



Rais Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Valentino Mlowola

UJENZI WA KIVUKO KIPYA KIGONGO BUSISI WAANZA RASMI



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu akiwa ameshikilia vifaa vya kuchomelea vyuma kuashiria kuanza kuweka msingi wa kivuko ‘’Keel Laying’’ katika eneo la Pasiansi ikiwa ni kumbukumbu ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu akichomelea vyuma kuashiria kuweka msingi wa kivuko ‘’Keel Laying’’ katika eneo la Pasiansi ikiwa ni kumbukumbu ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.



Meneja wa Miradi wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Major Songoro (kushoto) akitoa maelezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kulia) kuhusu kuanza kwa mradi wa ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.


Meneja wa Miradi wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Major Songoro (kulia) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto) michoro itakayotumika katika Ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.


Meneja wa miradi wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Major Songoro (kulia) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (katikati) michoro itakayotumika katika Ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Songoro Bwana Salehe Songoro. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Bwana Salehe  Songoro (wa pili kulia aliyenyoosha mkono) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (wa tatu kushoto) mojawapo ya malighafi itakayotumika katika ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.

Thursday 24 August 2017

FAMILIA YAGOMA KUMZIKA ANAYEDAIWA KUUAWA MGODINI GGM


Maeneo ya mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM)Shughuli zikiendelea za uchimbaji madini ya dhahabu.

Familia ya kijana Shija Charles mwenye umri wa miaka 25 imegoma kumzika ndugu yao huyo wanayedai kuwa amefariki baada ya kupigwa na walinzi wa mgodi wa dhahabu wa GGM na kutaka uchunguzi wa kina ufanyike.

BINTI AISHI KWA KUFUNGWA KAMBA MIGUUNI KWA MIAKA MITANO MKOANI GEITA




Lyaki Juma akiwa kwenye mazingira ya nyumbani kwao.



Binti Lyaki Juma akiwa amefungwa na kamba miguuni kwake ili hastoroke Nyumbani kwao. 

Msichana mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa mtaa wa nyakato Kata ya Ihanamilo kwenye Halmashauri ya mji wa Geita anadaiwa kufungwa kamba kwenye miguu yake kwa zaidi ya miaka mitano kutokana na tatizo la utindio wa ubongo.

Tuesday 22 August 2017

MBUNGE WA BUSANDA AMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUWAPATIA ENEO LA STAMICO WACHIMBAJI WADOGO


Mbunge wa Jimbo la Busanda Mkoani Geita,Loresia Jeremia Bukwimba amempongeza Rais kwa kutekeleza ahadi ya kuwapatia eneo la Stamico  wachimbaji  wadogo wa Kijiji Cha Nyarugusu 


Mbunge wa Jimbo la Busanda Lolesia Jeremia Bukwimba akikagua na kuangalia mwamba wa dhahabu wakati alipowatembelea wachimbaji wadogo wa mgodi wa STAMICO uliopo kwenye Kata ya Nyarugusu.


Baadhi ya wachimbaji wadogo wa maeneo ya STAMICO wakishangilia baada ya kutembelewa na Mbunge wa Jimbo la Busanda.


Wachimbaji wadogo wakimsikiliza Mbunge wakati alipokuwa akizungumza nao


Mchimbaji akimwonesha Mbunge Jiwe la mwamba wa dhahabu

VIWANDA 42 ZAIDI KUUNGANISHWA MFUMO WA GESI NCHINI



Serikali imesema kuwa viwanda vingine 42 vitaunganishwa na mfumo wa matumizi wa matunizi ya gesi asilia katika kipindi cha miaka miwili ili kuongeza tija tofauti viwanda 37 vya sasa ambavyo tayari vinatumia gesi hiyo.

WENYEVITI MHE. BALOZI ADADI NA MHE. BITEKO WAKUTANA NA WAJUMBE WA CHAMA CHA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA TAWI LA CANADA


Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Mhe. Yasmin Ratansi (wa pili kushoto) akizungumza pale ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Canada ambao ni Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ulipotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  leo Mjini Dodoma, ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi baina ya Mabunge hayo, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dotto Biteko, anaefuta ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu , kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Mhe. Kerry Diotte na katikati ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada Ndg. Remi Bourgaul



Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu (kulia) akizungumza pale ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Canada ambao ni Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ulipotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  leo Mjini Dodoma, ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi baina ya Mabunge hayo. Ujumbe huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Ndg. Yasmin Ratansi (wa pili kushoto), kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada ambae pia ni Mbunge, Ndg. Kerry Diotte na wa pili kulia, ni Katibu wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada Ndg. Remi Bourgault


Ujumbe wa Wabunge kutoka Bungela Canada ambao ni Wajumbe wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Tawi la Canada walipotembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Mhe.Yasmin Ratansi (watatu kushoto), Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mbunge wa Muheza, Mhe. Balozi Adadi Rajabu (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dotto Biteko (wanne kushoto) na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah (wa tatu kulia). Ujumbe ukiwa na lengo la kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi baina ya Mabunge hayo.


WADAU WA ZAO LA PAMBA WAKUTANA NA KUJADILI MBINU ZA KUBORESHA ZAO HILO MKOANI GEITA




Wakuu wa Wilaya zilizopo Mkoani Geita pamoja na wabunge na wadau wa Kilimo cha Pamba wakifuatilia kwa makini Mkutano  huo


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ,Dionis Myinga akijitambulisha mbele ya wadau wa sekta ya kilimo cha pamba.


Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza  kwenye mkutano wa wadau wa kilimo cha pamba

Wednesday 16 August 2017

KYUNGA AZIAGIZA HALMASHAURI KUTANGAZA VIVUTIO KWA WAWEKEZAJI GEITA




Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza  kwenye Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe.



Madiwani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita wakati alipokuwa akitoa maelekezo na ushauri.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Nicas Mayala akisisitiza kufanyia kazi ushauri ambao wamepatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita.


Mkurugenzi wa NGM GOLD MINE Emmanuel Gungu Siganga akipokea cheti cha Pongezi Kutoka kwa mmwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe kwa kuwa mdau mkubwa  wa kuchangia maendeleo kwenye sekta mbali mbali Wilayani Humo.



Baadhi ya wakuu wa Idara wakiwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani Wilayani Bukombe.

MBIO ZA MWENGE WA UHURU ZAMALIZIKA MKOANI GEITA

Mkuu wa Wilaya ya Magu akipokea mwenge wa uhuru kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati wa makabidhiano ya kimkoa.


Mkuu wa wilaya ya Magu Hadija Nyembo akisoma taarifa na shughuli ambazo zitafanywa na mwenge wa uhuru kwenye Mkoa wa mwanza.

KILA MWANANCHI NI LAZIMA APIMWE UKIMWI NCHINI ZAMBIA NA SIO HIARI TENA


Rais wa Zambia, Edgar Lungu, ametangaza kwamba wananchi wote wanaofika katika vituo vya afya vya serikali wapimwe virusi vya Ukimwi kwa lazima, wapatiwe ushauri nasaha na tiba.

MWANARIADHA ALPHONCE SIMBU APOKELEWA KWA SHANGWE NCHINI



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na baadhi ya Viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakimpongeza Mwanariadha Alphonce Simbu kwa kuibuka mshindi wa tatu ambapo alijinyakulia medali ya shaba. Hafla hiyo ilikuwa ni maalum ya kumpokea yeye pamoja na wanariadha wengine wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere toka nchini Uingereza kwenye Mashindano ya Marathon ya 2017.


Mwanariadha Alphonce Simbu akiwaonyesha Waandishi wa habari (hawapo pichani) medali ya shaba aliyoshinda katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka 2017.


Wazazi wa Mwanariadha Alphonce Simbu wakiwaonyesha Waandishi wa habari (hawapo pichani) medali ya shaba aliyoshinda mtoto wao katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka 2017.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na baadhi ya Viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) akipoka bendera ya Taifa toka kwa Wanariadha Aphonce Simbu na wenzake baada ya kuwasili toka nchini Uingereza kwenye Mashindano ya Marathon ya 2017.


Mwanariadha Alphonce Simbu akiwashukuru Viongozi mbalimbali waliokuja kumpokea na kumpongeza kwa ushindi wake katika Mashindano ya Mbio nchini Uingereza kwa mwaka 2017 ambapo aliweza kujinyakulia medali ya shaba