Wednesday, 30 March 2016

WANANCHI WILAYANI KARAGWE MKOANI KAGERA WATAKIWA KUTOCHUKUA SHERIA MKONONI.



Mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Karagwe mkoani Kagera amewataka wananchi  kutojichukulia sheria mkononi bali washilikiane na jeshi hilo kuwafichuwa wahalifu.


Wito huo umetolewa na kamanda wa jeshi la polisi wilayani humo Mika Makanja wakati akizungumza na chombo hiki ofisini kwake juu ya wananchi kujichukuliya sheria mkononi.

Kamanda Makanja amesema kuwa anawashukuru wananchi wa wilaya ya Karagwe kwa kutii sheria bila shuruti na kumaliza sherehe za pasaka bila kutokea tukio lolote lile.

Amesema kuwa wananchi wa wilaya hiyo wameanza kuelewa faida ya kushilikiana na jeshi la polisi katika suala la kuwafichuwa watu wanaovunja sheria za nchi  kwa kujichukulia sheria mkononi  hasa kwa kumpiga hadi kumuua mhalifu badala ya mtuhumiwa kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.


Hata hivyo amesema kuwa wananchi wa wilaya hiyo waendelee kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi wanapopata tetesi za kuwepo vitendo vya wizi na kuwafichuwa wahamiaji halamu .

No comments:

Post a Comment