Wananchi wa kata ya Kalangala
mtaa wa Misheni wilaya na mkoani
Geita wamelalamikia magari ya kubeba
taka kushindwa kubeba taka hizo kwa wakati hali inayoweza kuwasababishia kupata
magonjwa ya milipuko ukiwemo kipindupindu.
Wakizungumza na storm
habari wananchi hao wamesema kuwa magari hayo yamekuwa hayasimami mahali husika
kwa muda na na wakati mwingine huacha
taka hizo.
Naye mwenyekiti wa mtaa
huo bw. Juma Kajala amelalamikia swala hilo kutokutekelezwa huku akidai magari
hayo hayatekelezi majukumu yao kama wanavyokuwa wanazungumza kwenye vikao vyao.
“Magari yamekuwa
hayasimami mahali usika lakini pia yamekuwa hayakai mda mrefu nap engine kushindwa
kufika katika baadhi ya meneo jambo amblo linasabisha uchafu kuendelea kubaki
katika maeneo ya makazi ya watu”.alisema
Afisa mtendaji wa kata
hiyo Samsoni Lukas Muhondwa
amedai kuwepo kwa kero hiyo katika kata yake huku akiwalalamikia madereva hao kushindwa
kutekeleza zoezi hilo kwa wakati
Afisa usafishaji wa
mazingira wa halmashauri ya mji wa Geita Pankrasi Shwekelela
ametoa wito kwa jamii kutoa
ushirikiano kwa magari hayo huku
akidai mpango huo wa kupuliza filimbi ni mpya japo kuna changamoto
wanazokutana nazo madereva hao.
“Jambo hilo limekuwa likikubwa
na changamoto kwani mpango huu bado ni mpya hivyo watu wengi bado hawajaufahamu
vizuri ndio maana matatizo kama hayo yanajitokeza”,alisema
No comments:
Post a Comment