Thursday 31 March 2016

HIFADHI YA SAADANI YATEMBELEWA NA WAJUMBE WA KAMATI YA MALIASILI NA UTALII.


1.     Mkuu wa Hifadhi ya Saadani Bw. Hassan Nguluma akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Maliasili, Utalii na Ardhi ramani ya Hifadhi hiyo wakati kamati hiyo ilipoitembelea Hifadhi ya Saadani pamoja na kukutana na Menejimenti ya TANAPA. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani (mweye miwani) na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Atashasta Nditiye.

2.  Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe Atashasta Nditiye akizungumza na Menejimenti ya TANAPA wakati kamati hiyo iliopotembelea Hifadhi ya Saadani. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani

3.   Mkurugenzi wa Masoko na Utalii wa TANAPA Bw. Ibrahim Musa akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati hiyo ilikutana na TANAPA katika Hifadhi ya Saadani.

4.    Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati hiyo ilikutana na TANAPA katika Hifadhi ya Saadani.



MWENYEKITI WA KITONGOJI AUAWA BAADA YA KUFUMANIWA AKIFANYA MAPENZI NA MKE WA MTU VICHAKANI


Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bweya katika Kijiji cha Bweya mkoani Geita, Augustine Katemi (42) ameuawa baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mtu vichakani.

BINTI AJINYONGA HUKO LONGIDO ...AACHA MAJINA YA WATU ANAOWADAI NA KUAGIZA WALIPE KABLA MAITI YAKE HAIJASAFIRISHWA





Amesema amejinyonga kwa ridhaa yake mwenyewe.Katika ujumbe huo, ametaja majina ya watu anaowadai na kuagiza  walipe madeni yake kabla ya mwili wake kusafirishwa kwao pamoja na namba za Mama yake mzazi.

TAASISI NA MASHIRIKA MBALIMBALI YATAKIWA KUUNGA MKONO SEKTA YA ELIMU MKOANI GEITA.



Mkuu wa mkoa wa geita  meja Jenerali mstaafu Ezekile Kyunga, ametoa wito kwa taasisi,mashirika na watu binafisi kujitokeza katika kuunga mkono  swala la elimu  mkoani  hapa.

ASKARI POLISI ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUGUNDULIKA ALIJIPATIA AJIRA KWA VYETI VYA KUGUSHI.


Zoezi la kuhakiki watumishi hewa lililoamriwa na Rais John Magufuli limemkumba Askari Polisi aliyeajiriwa mwaka 2003 baada ya kubainika kuwa ametumia vyeti vya kugushi.

Wednesday 30 March 2016

WANANCHI WILAYANI KARAGWE MKOANI KAGERA WATAKIWA KUTOCHUKUA SHERIA MKONONI.



Mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Karagwe mkoani Kagera amewataka wananchi  kutojichukulia sheria mkononi bali washilikiane na jeshi hilo kuwafichuwa wahalifu.

SERIKALI MKOANI MWANZA KUBORESHA VIFAA VYA ULINZI NA USALAMA.


Serikali Mkoani Mwanza inatakiwa kuboresha vifaa vya  ulinzi na usalama katika visiwa vilivyo ndani ya ziwa Victoria ili kuweza kuinua huduma za uokozi na usalama wa raia mali zao visiwani humo.

AJALI YA MOTO YATOKEA MTAA BALENGE MKOANI GEITA NA KUTEKETEZA BAADHI YA VITU.

Ajali ya moto imetokea katika mtaa wa Balenge kata ya Kalangalala katika nyumba ya kulala wageni majira ya leo mchana wilayani na mkoani Geita na kusababisha uharibifu wa vitu vya thamani baada ya nyumba kuungua moto.

WATU WANNE WATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUTUMIA JINA LA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUTAPELI.



Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na tuhuma za kujipatia fedha kwa kutumia jina la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Tuesday 29 March 2016

AGIZO LA RAIS MAGUFULI KWA WAKUU WA MIKOA MWISHO LEO.

Rais waJamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli
Siku 15 alizotoa Rais John Magufuli kwa wakuu wa mikoa, wawe wamejumlisha wafanyakazi wote na kuhakikisha wanaondoa wafanyakazi hewa, zimetimia leo. Baadhi ya mikoa imeanika idadi ya watumishi hewa, waliobainika kupitia uhakiki huo, lakini mingi haijafanya hivyo.

RAIS MAGUFULI AZITAKA KAMATI ZA SHULE MKOANI GEITA KUSIMAMIA NIDHAMU NA UTORO SHULENI

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr, John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wilayani Chato mkoani Geita
Rais  wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr,John Pombe Magufuli amezitaka kamati zote za shule kuhakikisha kuwa zinasimamia swala la nidhamu na utoro katika shule  wanazoziongoza  na kama kuna kamati yoyote ambayo itashindwa ni vyema ikajihuzuru mapema.

RAIS MAGUFULI AWASILI LEO WILAYANI CHATO MKOANI GEITA KWA MARA YA KWANZA TANGU ACHAGULIWE KUWA RAIS.



Wakazi wa vitongoji mbalimbali wilayani Chato mkoa wa Geita,wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ambaye amewasili leo mjini humo alikozaliwa.Rais Dkt Magufuli amewasili wilayani Chato kwa mara ya kwanza tangu awe Rais.

PICHA:USIKU WA SNURA NA MSAMBWANDA DADAZ NDANI YA DESIRE PARK.


Dj Hk the Monster pamoja na Kg thedeejay wakifanya yao.

 Mwanakwetu Idrissa Salum akitahamaki mambo ya chura.

 Team ya kijiweni haikuwa mbali kuchukua matukio yaliyokuwa yakiendelea.


                               Mambo ya msambwanda dadaz yakihusika kwa stage.

 Washehereshaji wakifanya yo, huku Orest Ngowi hapa Mwanakwetu Idrissa Salum.

 Mofedha akikonga nyayo za mashabiki kwa stage.

 Baadhi ya mashabiki waliofika viwanja vya Desire park.

 Baadhi ya mashabiki waliofika Desire Park.

 Alianza chura mdogo kuruka stejini akafata chura mkubwa.

                                   Mashabiki wakionyesha support kwa snu sexy.


 Baadhi ya mashabiki waliojitokeza viwanja vya Desire Park.









Monday 28 March 2016

RAISI MAGUFULI AWATAKA WATANZANIA KUBORESHA USHIRIKIANO ZAIDI.


Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  Dkt.John Pombe Magufuli amewasihi watanzania kuendelea kuwa wamoja na kushirikiana kuijenga nchi yao badala ya kubaguana.

Ametoa wito huo katika kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Azania front jijini Dar es salaam, aliposali ibada ya pasaka pamoja na waumini wa  kanisa  hilo.

Amesema mwenyezi mungu alimtoa mwanae wapekee yesu kristo kuja kuikomboa dunia bila kuwabagua wanadamu, vivyo hivyo nasi binadamu wanapaswa kutobaguana, iwe kwa dini, makabila, mitazamo ya kisiasa na hata rangi  zetu.

Aidha  Rais Magufuli amewakumbusha watanzania kufanya kazi kama ambavyo vitabu vitakatifu vinasisitiza umuhimu wa kufanya kazi, na amebainisha kuwa tanzania yenye neema inawezekana endapo kila mtu atazingatia kufanya  kazi.

Katika hatua nyingine pia amewaomba watanzania kuendelea kuliombea taifa lao na pia kumuombea yeye ili afanikiwe kutekeleza jukumu kubwa na zito la kuiongoza   nchi pamoja na kuongoza maombi ya kumuombea Raisi Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli waliohudhuria ibada hiyo, Askofu mkuu wa KKKT Dayosisi ya mashariki na pwani Dkt.Alex Malasusa amempongeza Raisi magufuli kwa tabia yake ya kupenda kuhudhuria ibada na kuwasihi viongozi wengine kupenda ibada.


Askofu Malasusa ameuelezea ufufuo wa yesu kristo kuwa jambo la kuleta matumaini,na hivyo amepongeza mwelekeo wa nchi kwa sasa huku akisema kanisa linaona matumaini  kwa taifa.

Saturday 26 March 2016

SERIKALI MKOANI GEITA YAJIPANGA KUKABILIANA NA WATUMISHI HEWA

Mkuu wa mkoa wa Geita meja jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga
Serikali mkoani Geita, imejipanga vya kutosha kuhakikisha  kuwa inakabiliana na  watumishi hewa,ambapo ni agizo la raisi mh Jonh Magufuli la kuzitaka kila halmashauri nchini kushughulikia  tatizo  la watumishi  hewa.

VYOMBO VYA HABARI NCHINI VYATAKIWA KUELIMISHA WANANCHI KUHUSU UGONJWA WA KIPINDUPINDU.


Vyombo vya habari vimetakiwa kuelimisha wananchi kuchukua tahadhari  ya ugonjwa wa kipindupindu ambao tangu uanze miezi saba iliyopita bado upo na unazidi kuenea na kusababisha vifo.

SNURA A.K.A SNU SEXY NA MSAMBWANDA DADAZ KUKIWASHA KESHO PALE DESIRE PARK GEITA.


Ni ule usiku wa chura kuruka kichura chura kwa steji na kubwaga manyanga na zile zote kali za snura kama nimevurugwa, majanga, hawashi n.k zote zitahusika kesho tarehe 27 march pande zile za Desire park Geita.

Ni kwa mtonyo mdogo wa shilingi elfu tano tu unashuhudia mambo yote live, pia kumbuka ni kuanzia saa mbili kamili usiku hadi majogooo.

Njoo wewe,rafiki yako,na wengine wote tusheherekee sikukuu ya Pasaka. Usikose.


WATU WAWILI WAUAWA NA WENGINE SABA KUJERUHIWA JIJINI MWANZA.



Watu wawili wameuawa Jijini Mwanza kwa kupigwa risasi na Majambazi, huku Wengine saba wakijeruhiwa katika tukio la uvamizi wa duka lililokuwa likitoa huduma mbalimbali za kifedha.

PICHA:SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA BUNGE LA ISRAEL.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na  Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot (wa kwanza kulia) aliyemtembelea Ofisini kwake leo tarehe 26 Machi, 2016,Jijini Dar es Salaam.


Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot  aliyemtembelea Ofisini.


 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot  aliyemtembelea Ofisini.


  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la Israel, Ronen Plot  na viongozi wengine waliombatana na ujumbe huo.


Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Mzee Ibarahim Kaduma ambaye ni Mweyekiti wa Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT). Mzee Kaduma aliambatana na Ujumbe wa Israel uliomtembelea Spika ambao ndio wafadhili wa KLNT.

Friday 25 March 2016

ULINZI KUIMARISHWA MKOANI GEITA KWENYE SIKUKUU HII YA PASAKA.


Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi mkoani Geita, Mponjoli Lotson.

Jeshi la polisi mkoani Geita  limejipanga kuimarisha ulinzi  na usalama katika sikukuu ya pasaka itakayoadhimishwa jumapili march  27 duniani kote  ili kuwawezesha wananchi kusherehekea kwa amani na utulivu siku hiyo.

MIUNDOMBINU YA ELIMU NI TATIZO KUBWA SHULE ZA MSINGI MKOA WA GEITA.

Kufuatia agizo  la  serikali la kutoa elimu bure kuanzia ngazi ya msingi hadi kidato cha 4, baadhi ya shule za msingi mkoani hapa ikiwemo  Lutozo ,Ludete, na Nyawilimilwa zimeonekana kuandikisha idadi kubwa ya wanafunzi huku shule hizo zikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa walimu, madawati,  na vyumba vya madarasa hali ambayo inapelekea wanafunzi kusoma wakiwa chini ya mti na wakati mwingine hulazimika kurudi nyumbani pindi mvua zinaponyesha kutokana na kukosa mahali pa  kujikinga.

WATUMISHI HEWA 169 WAGUNDULIKA MKOANI KIGOMA.




Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Emanuel Maganga amewataka wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote waliopo katika halmashauri zote kutaja kiasi cha fedha kilichotumika kuwalipa mishahara watumishi hewa 169 kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Thursday 24 March 2016

MARCH 24 KILA MWAKA NI SIKU YA KIFUA KIKUU DUNIANI.




Kifua Kikuu (TB) ni ugonjwa ambao unafahamka kwa watu wengi  katika Tanzania kutokana na madhara mengi ambayo yamejitokeza na kuonekana iwe katika familia au katika jamii kwa namna moja au nyingine.

WANANCHI MKOANI GEITA WAMEIOMBA SERIKALI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSIANA NA UGONJWA WA KIFUA KIKUU

Wananchi  mkoani Geita wameiomba serikali  kutoa elimu zaidi kuhusiana na ugonjwa wa kifua kikuu ikiwa ni pamoja na watu kuhudhuria vituo vya afya kupima  ugonjwa huo.

Wednesday 23 March 2016

WATOTO WAWILI WA FAMILIA MOJA WAPOTEZA MAISHA BAADA YA KUZAMA KWENYE DIMBWI LA MAJI MKOANI GEITA.


Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Geita, Lotson Mponjoli


Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia  baada ya kuzama kwenye  dimbwi la maji  lililopo mtaa wa elimu,kata ya Nyankumbu mkoani Geita.

MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE SHULE YA MSINGI KALEMANI MKOANI GEITA AFANYIWA VITENDO VYA UBAKAJI KWA ZAIDI YA MIEZI MIWILI.


Mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi kilimani iliyopo mji mdogo wa Katoro wilayani Geita mwenye umri wa miaka 11 amekuwa akifanyiwa kitendo cha ubakaji kwa zaidi ya miezi miwili na mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Joseph.

Tuesday 22 March 2016

MARCH 23 YA KILA MWAKA WATU WOTE DUNIANI HUADHIMISHA SIKU YA HALI YA HEWA.


Tarehe ya 23 Machi kila mwaka Shirika la Hali ya Hewa Duniani(WMO) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali huadhimisha siku ya hali ya hewa Duniani. Maadhimisho haya ni kumbukumbu ya siku ya kuanzishwa kwa Shirika la Hali ya Hewa Duniani tarehe 23 Machi,1950.


WANAJUMUIYA WA KIKUNDI CHA UMOJA GROUP MKOANI GEITA KUPEWA PIKIPIKI NA DIWANI WA KATA YA BUKOLI.


Diwani wa kata ya Bukoli wilayani Geita Mhe.Faraj Rajab Seif  amewaahaidi usafiri   wa  pikipiki wanajumuiya ya kikundi cha kijamii kiitwacho “UMOJA GROUP” kilichopo kijiji cha Bugogo, kata  ya Bukoli ndani ya siku 30 toka machi 19, 2016.

WATU WAWILI WAPOTEZA MAISHA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KATIKA KATA YA LUDETE WILAYANI NA MKOANI GEITA.

                 Kamanda  wa jeshi la polisi mkoa wa geita Mponjoli Lotson.

Watu wawili wamepoteza maisha  kwa kupigwa na wananchi katika kata ya Ludete  wilayani na mkoani  Geita kwa kile kinachosadikika kuhusika katika tukio la kujaribu kuvamia katika nyumba ya Bw.Deusi  Francis mkazi wa kijiji cha Lwamgasa Mkoani hapa.