Karatasi za kupigia
kura kwa ajili ya uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar unaotarajiwa kufanyika
Machi 20, ziliwasili jana mchana visiwani hapa.
Karatasi hizo zilipokewa na watendaji mbalimbali wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), wakiongozwa na mkurugenzi wake, Salim Kassim katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Mkurugenzi huyo
aliwaeleza waandishi wa habari kuwa jumla ya karatasi 5,385 ndizo zilizowasili.
Kassim alisema
karatasi hizo zimechapishwa katika kiwanda cha Unprint cha Durban, Afrika
Kusini na ziliwasili hapo kwa ndege yenye Na EW-364TG ya nchi hiyo. Alisema
karatasi hizo pamoja na vifaa vingine vitasambazwa vituoni Machi 18, mwaka huu.
Kassim alisema katika
karatasi hizo za kupigia, yapo pia majina ya wagombea wote tisa wa vyama vya
upinzani waliokwishatangaza kutoshiriki uchaguzi huo wa marudio.
Miongoni mwa wagombea
hao ni Maalim Seif Sharif Hamad wa CUF, ambaye ametangaza kujitoa.
Uchaguzi huo wa
marudio, pia unaelezwa kugomewa na waangalizi wa kimataifa na hata wale wa
ndani.
Mbali na CUF vyama
ambavyo pia vimeeleza kutoshiriki uchaguzi huo ni Chaumma, Chama cha Kijaamii
(CCK), APPTMaendeleo, ACT-Wazalendo, Jahazi Asilia, Demokrasia Makini, NRA na
SAU.
Kassim alipotakiwa
kueleza sababu za ZEC kuchapisha karatasi za kura zenye wagombea waliotangaza
kususia uchaguzi huo wa marudio, alijibu kuwa yeye si msemaji.
Akizungumzia gharama
za uchaguzi huo wa marudio, mhasibu wa ZEC, Yussuf Ali Hassan alisema
utagharimu Sh4.5 bilioni tofauti na ule wa Oktoba 25, mwaka jana uliofutwa
ambao uligharimu kiasi ya Sh5.3 bilioni.
Picha za ujio wa
Makatarsi na huyo anayeonekana hapo ni Mkurugenzi wa ZEC Salim Kassim Ali
akitoa maelezo ya kuwasili kwake uwanja wa ndege Zanzibar.
No comments:
Post a Comment