Mahakama ya wilaya ya Bukombe
mkoani Geita imewahukumu watu wanne
kwenda kutumikia kifungo cha miaka minne
jela kila mmoja kwa kosa la wizi wa pikipiki aina ya sanilg.
Waliohukumiwa kifungo jela ni Marco Emanuel Teso mkazi wa Katoro na wenzake watatu ambao ni Elisha John naye ni mkazi wa Katoro na wengine ni Paskal Hamis mkazi wa Katente na Nelson Mandela mkazi wa Kapera mjini Ushirombo.
Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa
mahakama hiyo Gabriel Kurwijila mwendesha mashtaka wa polisi Elias Mgobera
aliiambia mahakama hiyo kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo julai 6 mwaka jana majira ya saa
nane usiku huko mtaa wa Kapera Masakuroni ambako
walifanya njama na kuiba pikipiki aina ya sanilg yenye usajiri namba t192 adl
mali ya Andrew Jackson yenye thamani ya sh. milioni moja laki saba na tisini
1,790,000 .
Baada ya mahakama kuridhika na
ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka na wao kukiri kuwa
walifanya njama hakimu Gabriel Kurwijira amewahukumu wote wanne kwenda
kutumikia kifungo jela miaka minne kila mmoja na baada ya kumaliza kifungo
watawajibika kulipa kila mmoja sh.laki nne arobaini na saba na miatano (447,500) ili kulipa pikipiki ,
chini ya kifungu 258 na 265 kanuni ya adhabu sura namba 16 ili iwe fundisho kwa
wengine kutokana na matukio ya wizi wa pikipiki kukithiri wilayani Bukombe.
No comments:
Post a Comment