Akipunga mkono na mkewe mara baada ya kuwasili nchini.
Waziri mkuu, Mh. Kassim Majaliwa akimpokea mara baada ya kuwasili jana.
Mh.Truong Tan Sang akishuka kwenye ndenge na mkewe mara baada ya kuwasili nchini katika uwanja wa J k Nyerere jijini Dar es salaam.
Raisi wa Jamhuri ya
Kisoshalisti ya Vietnam, Truong Tan Sang, amewasili nchini
jana saa mbili usiku tayari kwa kuanza ziara ya siku
tatu nchini, ambapo pamoja na masuala mengine, atasaini mkataba wa masuala ya
Kodi na mwenyeji wake Rais John Magufuli.
Mkataba huo unalenga kuchochea biashara kati ya Vietnam na Tanzania kwa kuwa utatoa fursa kwa wafanyabiashara wa pande zote kutotozwa kodi mara mbili katika biashara na uwekezaji watakaoufanya.
Rais huyo anatarajiwa
kupigiwa mizinga 21 leo, ikiwa ni pamoja na kukagua gwaride rasmi, ambapo
baadaye atatambulishwa kwa viogozi mbalimbali wa Serikali, kabla ya kufanya
mazungumzo na Rais Magufuli.
Kwa mujibu wa ratiba
iliyotolewa Dar es Salaam kuhusu ujio wa Rais huyo wa Vietnam, baada ya
viongozi hao kutia saini mkataba huo, mgeni huyo na ujumbe wake atakwenda
kwenye ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyopo katika Mtaa wa Lumumba
jijini humo kukutana na Mwenyekiti wa chama hicho, ambaye ni Rais mstaafu wa
Tanzania, Jakaya Kikwete.
Rais huyo wa Vietnam
ambaye ni mmoja wa viongozi waandamizi wa Chama cha Kikomunisti cha nchi hiyo
chenye uhusiano wa muda mrefu na CCM, atakwenda kwenye Mamlaka ya Ukanda
Maalumu wa Uwekezaji (EPZA) Ubungo, Dar es Salaam kutembelea viwanda na kupata
taarifa za fursa za uwekezaji katika sekta ya viwanda nchini.
Aidha, ratiba hiyo
imeeleza kuwa atahudhuria mkutano wa biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo
mbili, kabla ya kukutana na Spika wa Bunge, Job Ndungai na Rais wa Zanzibar, Dk
Ali Mohamed Shein katika wakati tofauti.
Pamoja na ujumbe wake
atatembelea hifadhi ya wanyama ya Saadan iliyoko Bagamoyo na kuondona nchini
Machi 11 kuelekea Msumbiji kuendelea na ziara yake.
No comments:
Post a Comment