Baadhi ya wachimbaji wakifanya jitihada za kuokoa watu waliofukiwa na kifusi Mgusu mkoani Geita |
Watu watano wamefariki dunia na wengine wanne
wamejeruhiwa vibaya baada ya kuangukiwa na kifusi wakati walipokuwa kwenye shughuli za uchimbaji madini katika
kata ya Mgusu wilayani na mkoani Geita.
Tukio hilo limetokea
jana mnamo majira ya saa tisa alasili ambapo wachimbaji hao walifukiwa
pindi walipo kuwa katika shughuli hiyo.
Akithibitisha
kupokea miili hiyo mganga mfawidhi wa hospitali teule ya rufaa mkoani hapa bw,
Adamu Sijaona amesema walio poteza maisha ni pamoja na Kazimili Seni umri miaka
55,Eva Moshi Maduhu umri miaka 23,Washima Makonda umri miaka 44,Shija Solo umri
miaka 46 na Bahati Sipringi umri miaka 35 lakini kwa upande wa majeruhi ni
Mboke Upepu umri miaka 30,Nkwimba Semi umri mika 54,Saimoni Jonathani umri miaka 23
Aliongeza kuwa majeruhi hao wamevunjika baadhi ya
viungo vya mwili pindi walipo fukiwa na kifusi.
Baadhi ya wakazi walio shuhudia tukio hilo wamesema
kuwa eneo hilo lilikuwa limezuiwa lakini baadhi ya watu walikaidi na wakawa
wana ingia kuchimba pasipo kuruhusiwa ,hata hawa walio poteza maisha walitumia
njia za kinyemela kuingia katika eneo
hilo.
Kwa upande wake bw,Msimu Kabasa ambae ni fundi sanifu
migodi ofisi ya madini Geita amesema
kuwa hapo awali serikali ilitoa taarifa ya kuzuia shughuli za uchimbaji lakini baadhi ya wachimbaji walikaidi agizo hilo.
Bw,Kabasa alitoa kauli ya kulifungia eneo hilo kwa
muda usiojulikana hadi pale serikali itakapo jirizisha kwa uchunguzi zaidi.
Aidha kaimu afisa madini wa mkoa wa Geita bw
Fabiani Lukas alifika katika eneo la tukio nakusema kuwa tatizo kubwa la wananchi wamekuwa hawatii
maagizo ambayo yana tolewa na serikali
kwani eneo hilo walilizuia tangu awali
kwasababu lilikuwa hatarishi lakini wachimbaji hawakutaka kutii agizo hilo
ambapo pia amewataka wananchi kwa ujumla wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji
kuwa na tabia ya kuwasikiliza viongozi wao pindi watoapo maagizo.
No comments:
Post a Comment