Kampuni ya Trumark hapa Tanzania
inaandaa Tamasha la Pamoja Tunafanikisha kusherekea Siku ya Wanawake duniani
Machi 8, mwaka huu. katika Ukumbi wa King Solomoni, eneo la Namanga jijini Dar
es salam. Siku hii muhimu itawakutanisha wanaume na wanawake wataungana
kusherekea mafanikio ya wanawake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark
Bi Agnes Mgongo alisema kwa kutambua changamoto nyingi zinazomkabili mwanamke,
katika kuadhimisha siku hiyo Trumark imekuwa ikiandaa shughuli za maadhimisho
kwa kuwaalika wadau mbalimbali kutoka nyanja tofauti ili kujadiliana namna ya
kuzikabili na kuzifanya kuwa fursa na pia kuwapongeza wanawake ambao
wameonyesha njia kwa kujikwamua kiuchumi, kijamii na kiafya huku kauli mbiu ikiwa "50-50 MPAKA KUFIKIA 2030"
Trumark imekua ikiadhimisha siku
ya wanawake kwa takribani miaka mitano sasa na tumekuwa na mafanikio makubwa
kwani washiriki wengi wamekuwa na mrejesho chanya, nakuongeza mtandao katika
shuguli zao mbalimbali.
Aliongeza Bi Agnes alisema hii
inakuja ikiwa ni mwaka wa kwanza baada ya umoja wa Mataifa (United Nation) kuja
na malengo mapya 17 ya maendeleo endelevu (SDGS) baada ya kuisha muda kwa
malengo nane ya millennia yaliyowekwa na umoja huo mwaka 1990. Katika malengo
haya mapya lengo namba 5 linataka kuleta usawa wa kijinsia na kuwawezesha
wanawake na wasichana kila mahali.
Katika kuelekea maadhimisho ya
siku ya mwanamke duniani, mwanamke wenyewe anayo fursa kubwa ya kujitathimi na
kujitambua anahitaji nini katika maisha yake Alisisitiza kweli nguvu za pamoja
zinahitajika ili kumwezesha mwanamke kutoka mahali aliko sasa, lakini hilo
litafanikiwa zaidi ikiwa mwanamke naye atachukua hatua ya kujitoa kitanzini kwa
kushirikiana na mwanaume.
Hivyo ni swala la jamii nzima
kushiriki harakati hizi za kuleta usawa wa kijinsia. Alisema maadhimisho
yataambatana na burudani kutoka kwa wasanii wa bendi ya mapacha watatu pamoja
na chakula cha usiku katika kusheherekea mafanikio ya wanawake.
Agnes alifafanua kuwa wageni
waalikwa watapata fursa ya kuhamasishw a maswala ya afya ikiwemo faida ya
mazoezi ili kujenga afya bora na kuepukana magonjwa yale yasiyo ambukizwa
lakini ni hatari kama kisukari, shinikizo la damu na uzito uliozidi (obesity).
Pia aliongeza katika siku hiyo
kutakuwa na fursa kwa wafanyabiashara wanawake kujitangaza kwa kufanya
maonyesho ya bidhaaa zao mbalimbali (exhibition) ili kujitangaza na kujiongezea
wateja.
Aliwakaribisha wahisani na wadau
mbalimbali wanaojihusisha na maswala mbalimbali ya Wanawake kujitokeza na
kushiriki pamoja katika siku hii muhimu kwa jamii yetu. Pamoja wanaume na
wananake Tunafanikisha mafanikio ya wanawake.
No comments:
Post a Comment