Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi mkoani Geita, Mponjoli Lotson.
Jeshi la polisi mkoani Geita limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama katika sikukuu ya pasaka itakayoadhimishwa
jumapili march 27 duniani kote ili kuwawezesha wananchi kusherehekea kwa
amani na utulivu siku hiyo.
Akizungumza na storm habari ofisini kwakwe kamishina
msaidizi wa jeshi la polisi mkoani hapa, Mponjoli Lotson amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kugundua
kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakitumia mwanya huo kufanya uhalifu kutokana na
kuwepo kwa muingiliano mkubwa wa wananchi katika sehemu mbalimbali.
Aidha kamanda Mponjoli amebainisha kuwa maeneo yote
wameimarisha ulinzi ikiwemo kumbi za starehe, makanisa, sehemu zote za
njia kuu, huku askari wakipangwa kila
mitaa.
Aidha kamanda amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa
jeshi la polisi kwa kutoa taarifa sehemu husika pindi wanapokuwa na na mtu
ama kikundi cha watu.
No comments:
Post a Comment