Friday 30 March 2018

MGODI ULIOUA WACHINA MKOANI GEITA WAFUNGWA



Mgodi  wa dhahabu katika Kijiji cha Nyamtondo wilayani na mkoani Geita umefungwa baada ya raia wawili wa China kufariki ndani ya shimo lenye urefu wa zaidi ya mita 100 kwa kulipukiwa na baruti wakati wakivunja miamba.

NDEGE YA TANZANIA AINA YA BOMBARDIER Q400 ILIYOKUWA IMEZUILIWA NCHINI CANADA IMEKWISHAONDOKA KUJA NCHINI


Kwa Mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Gerson Msigwa amesema Ndege ya Tanzania iliyokuwa inashikiliwa nchini Canada imeshaondoka nchini humo na inarejea Tanzania.

Msigwa ameandika hayo kupitia ukurasa wakwe wa mtandao wa kijamii wa Twitter

Pia Msigwa ameongeza kuwa Ndege 3 kubwa, Mbili aina ya Bombardier CS300 kutoka Canada na Moja Boeing 787-8 Dreamliner kutoka Marekani zitawasili baadae mwaka huu


"Ndege yetu aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imezuiliwa nchini Canada ilikwishaondoka Canada kuja Tanzania. Aidha, ndege kubwa nyingine 3 (2 Bombardier CS300 kutoka Canada & 1 Boeing 787-8 Dreamliner kutoka Marekani) zitawasili baadaye mwaka huu. Nawatakia Ijumaa Kuu njema."-Msigwa

Thursday 29 March 2018

CAG AOMBA RADHI KUHUSU TAARIFA YA UKAGUZI ALIYOIWASILISHA KWA RAIS MAGUFULI


Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Profesa. Mussa Assad ameomba radhi wananchi na serikali juu ya taarifa ya deni la taifa na kusema kuwa yalifanyika makosa ya kimatamshi, deni hilo ni himilivu.

Profesa Assad ametoa taarifa hiyo mjini Dodoma ambapo amesema deni halisi ni shilingi trillion 46.08 na ni himilivu hivyo anaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa wananchi na taasisi za serikali.

CAG wakati akitoa ripoti hiyo kwa Rais John Pombe Magufuli kuhusu suala la muenendo wa deni la taifa alidai kuwa deni la taifa si himilivu lakini kwa mujibu wa utafiti ambao wamefanya wao CAG ameibuka na kuomba radhi na kusisitiza kuwa ripoti ya CAG ni siri hadi itakapowasilishwa bungeni.  


UHABA WA VYOO SHULE YA SEKONDARI LUBEMBELA WAWALIZA WANAFUNZI




Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lulembela iliyopo kata ya Lulembela Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita wanalazimika kukimbilia vichakani kwenda kupata huduma ya choo kutokana na shule hiyo kukabiliwa na uhaba mkubwa wa matundu ya vyoo.

BAADHI YA MAKAZI WILAYANI CHATO YAHARIBIWA NA MVUA








Zaidi ya kaya 139 katika kijiji cha mkuyuni kata ya chato wilayani chato mkoani Geita zimekumbwa na mafuriko ya maji kufuatia mvua zinazo endelea kunyesha huku kaya 24 kati ya hizo zikikosa mahala pakuishi baada ya nyumba zao kubomoka.

RC MASENZA AWAPONGEZA RDO KWA KUTATUA TATIZO LA MAJI KWENYE BAADHI YA VIJIJI VYA WILAYA YA MUFINDI NA KILOLO


 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi.


 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akimtusha ndoo ya maji mmoja ya wananchi walihudhulia uzinduzi wa mradi maji ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania


 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania Fidelis Filipatali wakibadilisha mawazo juu ya mradi huo ambao umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100)


 Hapa ndio tank kubwa la mradi wa maji unaofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania na 
umegharibukiasi cha shilingi milioni tisini na tano,laki tano na elfu tatu mia moja ( 95,503,100)


Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Nandala alipokuwa ameenda kuzindua mradi wa maji ambao utasaidia kupunguza changamoto ya maji na kuchochea maendeleo kwa wananchi ambao watakuwa wananufaika na mradi huo ulifadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania ambao makao makuu yao yapo Mdabulo Mufindi.

Wednesday 28 March 2018

WANANCHI WATAKIWA KUNUNUA HISA NA HATI FUNGANI ILI KUNUFAIKA KIUCHUMI

Baadhi ya wadau wakiwa kwenye mafunzo ya ununuzi wa hisa ambayo yamefanyika kwenye ukumbi wa maarifa ya Nyumbani Mjini Geita.

Meneja Mahusiano ya Umma wa CMSA Bw Charles Shirima akifundisha namna ya uwekezaji wa hisa. 



Serikali kupitia mamlaka ya masoko ya dhamana na mitaji nchini ya Capital Markert and Securities Authority, CMSA imesema ununuzi na uuzaji wa hisa na Hati fungani za makampuni na serikali ni mbinu nzuri za kujiwekea akiba na kumfanya mtu kutajirika.

VIONGOZI WA KIKRISTO MKOANI GEITA WAHIMIZA AMANI NA UTULIVU KWENYE PASAKA

Image result for KANISA


Baadhi ya Viongozi wa Kikristo mkoani Geita wamewataka Wakristo kusherehekea Sikukuu ya Pasaka kwa amani na utulivu na kujiepusha na matendo maovu wakati wa sherehe hizo.

Padri Gerald Singu ambaye ni Paroko wa Parokia ya Bikra Maria wa Fatima Geita, Mchungaji Gerson Yoboka ambaye ni kiongozi mkuu wa kanisa Anglikana mkoani Geita na Mchungaji Mathias Michael Kasente wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, KKKT Usharika wa Upendo wametoa kauli hiyo walipokuwa wakitoa ujumbe wao wa Pasaka kwa Waamini.

Wamesema ni vema Wakristo wakabadilika na kuacha dhambi badala yake wafanye mambo ya kumpendeza Mungu na kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakipania kufanya matendo maovu katika Sikukuu mbalimbali.

WATAALAM WA MADINI YA DHAHABU NCHI ZA UKANDA WA MAZIWA MAKUU (ICGLR) WAKUTANA ARUSHA




Baadhi ya Waratibu wa Mkutano wa Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakifuatilia majadiliano kwenye mkutano huo Jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi wa Demokrasia na Utawala Bora- ICGLR,



Balozi Ambeyi Ligabo akifuatiwa na Mwenyekiti wa Mkutano, Service Julie kutoka Congo.


Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiendelea na majadiliano



Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiendelea na majadiliano Jijini Arusha.

JESHI LA POLISI MKOANI GEITA LAJIPANGA VIKALI DHIDI YA MAANDAMANO





Jeshi  la polisi mkoani Geita , limewataka  wananchi  katika kuelekea   siku kuu ya pasaka pamoja na uzinduzi wa mwenge Kitaifa, kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na wazazi kuhakikisha usalama na watoto  wanapokuwa kwenye maeneo ya barabara na mitaani.

JESHI LA POLISI MKOA WA GEITA LIPO IMARA KUDHIBITI UHALIFU NA MAANDAMANO APRILI 26



Jeshi  la polisi mkoani Geita , limewataka  wananchi  katika kuelekea   siku kuu ya pasaka pamoja na uzinduzi wa mwenge Kitaifa, kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na wazazi kuhakikisha usalama na watoto  wanapokuwa kwenye maeneo ya barabara na mitaani.

Monday 26 March 2018

UVCCM GEITA YAWAKUTANISHA WATU WENYE ULEMAVU WANAWAKE NA VIJANA KUJADILI ASILIMIA 10 ZINAZOTOLEWA NA HALMASHAURI

Wajumbe wa mkutano ambao ulikuwa umelenga kutoa ufafanuzi juu ya asilimi 10 ambazo zinatolewa na halmashauri kwa wanawake,vijana pamoja na walemavu Wilayani Geita.

Katibu wa UWT,Bi Mazoea Salum akielezea akisoma mapendekezo ambayo wameyaadhimia kwenye Kikao hicho.

Katibu wa chama cha mapinduzi(CCM) Wilaya ya Geita,Julius Peter Akizungumza na wajumbe kwenye mkutano huo.

Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye Kongamano hilo akisisitiza suala la uanzishwaji wa viwanda vidogo kwenye vikundi.

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Geita,Manjale Magambo akielezea umuhimu wa fedha asilimia 10 ambazo zimekuwa zikitolewa na halmashauri kwa vikundi vya vijana ,wanawake na walemavu.

WAWEKEZAJI WAZAWA WAPEWA RAI KUJENGA VIWANDA VYA DAWA



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Global Fund Linden Morrison wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Waziri wa wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Madawa, Laurean Bwanakunu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.




Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Madawa, Laurean Bwanakunu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.




Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya  magari 181 yatakayokuwa yatayosafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa hafla ya  magari 181 yatakayokuwa yatayosafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari 181 yatakayokuwa yatayosafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,. Jinsia, Wazee na Watoto akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishuka katika moja ya magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mwakilishi wa Global Fund na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.



Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mwakilishi Mkazi wa Global Fund, Linden Morrison wakifurahia jambo na wafanyakazi wa Bohari Kuu ya Madawa (MSD) mara baada ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.




Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikagua baadhi ya magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam

Friday 23 March 2018

WANANCHI WALIA NA MKANDARASI WA BARABARA GEITA

Barabara inayotoka amerikani Chips Kuelekea Jimboni ikiwa kwenye hatua za awali za ujenzi.
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza suala la mkandarasi kushindwa kutekeleza ujenzi wa Barabara kwa wakati.
Baadhi ya maeneo ambayo wananchi wameendelea kulalamika kuathiriwa na mvua kutokana na kifusi ambacho kimewekwa na mkandarasi kwenye Barabara ya Amerikani Chips  inayoenda Jimboni.
Bi,Getruda Daud ambaye ni mkazi wa Katundu akilalamika namna ambavyo wameendelea kupata shida kutokana na kushindwa kukamilika kwa ujenzi wa Barabara pamoja na daraja.
Baadhi ya wananchi wakiangaika kuvuka kwenye kidaraja kidogo kutokana na kushindwa kukamilika kwa Daraja.

Nyumba ikiwa imeenea maji kutokana  na kifusi ambacho kimelalamikiwa na wananchi.